Na Joel Maduka Geita..
Kiasi cha Sh,Milioni 4 ambazo zimetolewa na Chama cha Mapinduzi(CCM) tawi la Ihayabuyaga Mtaa wa Ujamaa Kata ya Kalangalala ,Wilayani geita kwa ajili ya Bima ya afya iliyoboreshwa (CHF) lengo likiwa ni kuwapatia wananchi wasio jiweza waweze kupata huduma bure za afya kwa mwaka mzima.
Akikabidhi bima hizo kwa wananchi Mwenyekiti wa Umoja wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Geita Manjale Magambo amewataka ametoa wito kwa wananchi kujiunga kwa wingi kwenye mfuko wa Bima ya Afya ulioboreshwa ili wapate vitambulisho vitakavyowasaidia kupata matibabu kwa mwaka mzima katika vituo vya kutolea huduma ikiwemo na Hospitali za Rufaa.
Amesema serikali imeendelea kujali afya za wananchi, huku akitumia jukwaa hilo kuipongeza CCM tawi la Ihayabuyaga kwa kujitolea kulipia Bima 120 zilizogharimu zaidi ya Sh. Milioni 4 ambapo wakazi wa Mtaa wa Ujamaa watanufaika kwa Mwaka mzima.
“Ndugu zangu wananchi Mhe Rais anatengeneza mazingira bora ya afya sasa niwaombe sana sisi wajibu wetu mkubwa ni kukata bima ya afya iliyoboreshwa na gharama zake ni nafuu sana,lakini niwapongeze CCM Tawi la Ihayabuyaga kwa kuja na maono ya kuwasaidia wazee wetu kupata bima ya afya kwani mmejichanga na kujibana mkatambua mchango mkubwa walionao wazee kwenye Taifa mkawakatia bima nawapongeza sana”Manjale Magambo Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita.
Sanjali na Hayo Mwenyekiti wa UVCCM Geita Manjale Magambo amewaomba wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani katika mapambano ya kuleta maendeleo.
Antony Ndega ni Katibu wa CCM Tawi la Ihayabuyaga amesema waliamua kujichangisha kupitia miradi waliyonayo kwa lengo la kutambua umuhimu wa wazee na jitihada za afya ambazo zinafanywa na serikali na kwamba kupitia msaada huo wa bima za afya zilizoboreshwa walizozitoa ni moja ya jambo muhimu la kumuunga mkono Mhe ,Rais Samia Suluhu Hassan katika uboreshaji wa afya.