Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu amesema serikali ya Tanzania itashirikiana na Somaria katika kutoa mafunzo ya ubigwa na ubigwa bobezi kwa wataalamu wa afya wa Somalia kwani nchi imefanya vizuri katika kuboresha huduma za ubigwa na ubigwa bobezi hasa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete(JKCI),Hospital ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Mifupa (MOI)
Amesema nchi ipo vizuri na inavifaa tiba vya kisasa na Madaktari Bigwa na Bobezi ambao wamejengewa uwezo na wanauzoefu mkubwa katika kutoa huduma za afya.
Waziri Ummy ameyasema hayo Aprili 27, 2024 wakati wa ziara ya Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Dkt. Hassan Sheikh Mahmoud alipotenbelea katika Bohari Kuu ya Dawa ya Taifa MSD Keko jijini Dar es salaam.
Amesema pia watashirikiana katika mafunzo ya wataalam wa afya kwani wao wanaoshia katika ngazi digrii ya kwanza hivyo kupitia kwenye Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) katika kuwafundisha wataalam wa afya kutoka Somalia katika maeneo hayo ya ubingwa na ubingwa bobezi.
Amesema lakini pia watashirikiana katika swala la usambazaji na ununuzi wa dawa kupitia Bohari Kuu ya Dawa MSD kwani bohari hiyo imekuwa na uzoefu mkubwa.
“MSD imekuwa na uzoefu mkubwa katika kununua,Kutunza na kusambaza dawa kwani wanahudumia zaidi ya vituo 8000 nchini Tanzania”,Amesema Ummy
Aidha ameongeza kuwa Mawaziri wa SADC waliipa MSD dhamana kununua dawa kwa niaba ya nchi nyingine za SADC na kazi hiyo imekuwa ikifanyika kwa ufanisi mkubwa na MSD.
Amesema kwa kuwa sasa Somalia ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo wanaweza kushirikiana nao kuhakikisha wananunua dawa kwa pamoja ili kupata dawa zenye ubora na kwa bei rahisi na kuzipeleka Somalia.
“Lengo la ziara ya Rais wa Somalia MSD ni kuona kwa vitendo shughuli za MSD lakini pia tumepokea maelekezo kutoka kwa wakuu wetu wa nchi kuwa mawaziri wa pande zote tukae na tuangalie namna ambavyo tunaweza kuanza utekelezaji wa maswala haya”,Amesema Waziri Ummy Mwalimu.