Na Sophia Kingimali.
Mkurugenzi wa Furaha Media Dominic Furaha ametoa rai kwa wananchi ambao wanakipato pamoja na viongozi kuwasaidia wahitaji kwani kwa kufanya hivyo ni kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika jitihada zake za kusaidia wanyonge na wenye uhitaji.
Wito huo ameutoa April 27,2024 Jijini Dar es salaam wakati akitoa msaada wa vitu mbalimbali kwa famili ya Bwana na Bibi Elijah wanaolea watoto waliotoka kwenye mazingira hatarishi lakini pia katika kituo kinacholea watoto yatima cha Faraja kilichopo Mburahati jijini hapo.
Amesema watoto wote nchini ni sawa hivyo jamii inapaswa kuwalea na kuwalinda ili kuhakikisha wanapata haki zao za msingi ambapo kwa kufanya hivyo ni kusapoti juhudi za Rais Dkt Samia za kataka kumuwezesha mtoto wa kitanzania kufikia malengo yake.
“Tumeona serikali yetu chini ya uongozi Rais Dkt Samia Suluhu Hassan umeongeza idadi ya shule lakini kufuta karo zote za shule na mtoto kusoma bure kuanza la kwanza hadi elimu ya juu sasa kama jamii kazi yetu ni kuhakikisha hawa watoto wanapata mavazi,uniform madaftari Mabegi na vitu vingine ili na wao wajione kama watoto zetu majumbani”
Aidha Furaha ameongeza kuwa unapotoa kwa ajili ya muhitaji pia unaongeza nafasi yako ya kufanikiwa na kukumbukwa na Mungu na hiyo ndio siri yake kubwa ya mafanikio katika maisha yake.
Amesema kutokana na maisha yake aliyokulia anapata faraja pindi anapokutana na watu ambao wanapitia maisha ambayo yeye aliyapitia katika kipindia ambacho alichokuwa anakuwa kwani aliachwa na wazazi wake akiwa na miaka mitatu na walilejea akiwa mkubwa hivyo mtaa ndio ulimlea.
“Ninapowaona hawa najiona mimi na ndio maana ninapata faraja kubwa na furaha pindi ninapokuwa nao napenda kuwatia moyo sana na nitoe rai kwa wengine kufanya hivi au kutenga angalau asilimia moja kwa pesa wanazotumia ili kuwalete hawa maana wanapowashukuru na kuwaombea dua ndio mafaniko yao”,Amesema.
Aidha Furaha amesema kuwa anaovijana ambao amewachukua kama watoto wake ambao anawasomesha na wapo katika madaraja tofauti anao wa sekondari mpaka vyuo vikuu na bado ataendelea kufanya hivyo na kuwafanya kuwa familia yake.
Kwa upande wake Dkt Consoler Eliya ambae ni mama anaelea watoto 60 ambapo kati ya hao wawili ndio wakwake wa kuzaa na 58 wakulea amesema amekuwa akifanya hivyo kwa miaka 19 sasa.
Amesema jamii inapaswa kulea watoto yatima na wanaotoka kwenye mazingira hatarishi kama wapo nyumbani ili kuwafanya na wao kufurahia maisha hali itakayowapelekea kuweza kutimiza ndoto zao.
“Kukaa na watoto hii ni moja ya ndoto zangu mimi ni mama wa watoto 60 nawafurahia nawalea na kuwatunza ninawatoto wanaosoma kuanzia shule ya msingi mpaka vyuo na wapo ambao tayar wamehitimu mimi na mume wangu tunajivunia hili na ndio maana tangu mlipotokea uwezi kuona kibao kinaonyesha hapa nalea watoto yatima hawa ni wanangu na hapa wapo nyumbani kwao”,Amesema.
Sambamba na hayo amemshukuru Mkurugenzi wa Furaha Media kwa kuwajali na kuwaletea vyakula pamoja na vifaa vya shule kama madaftari,soksi na peni pamoja nakuweza kuwalipia umeme wa.miezi sita,nauli za shule za wanafunzi na kuwachangia kwenye mfuko wa elimu.
Naye,mkuu wa kituo cha Faraja Bahata Kajongo amemshuru Mkurugenzi huo kwa kuweza kuwapa msaada huo lakini kula pamoja na watoto kwani watoto wamefarijika na kufurahi kwa kitendo hicho.
“Tunamshukuru sana bwana Furaha sisi tunamuita Fahad kwa kujumuika na watoto na tunamuombea Dua kwa Mungu azidi kumfanikisha na kumlinda na kila baya ili aendelee kusaidia wahitaji kwenye maeneo mbalimbali ya nchi yetu”,Amesema.
Furaha Dominic ambae ametambulisha jina lake jipya la Fahad akiwa na wafanyakazi wa taasisi yake wametembelea vituo hivyo na wametoa misaada mbalimbali ikiwa kama sehemu ya shukrani kwa Mungu lakini kuhakikisha wanatoa Furaha kwa wananchi wote.