Timu ya Mpira wa Miguu FGA ya Songea imeipa kichapo cha goli 3-1 Timu ya Mbeya City katika mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa leo Aprili 27, 2024 katika uwanja wa Majimaji Songea.
Katika mchezo huo wa kukata na shoka kila timu imeonesha ushindani wa kusaka alama tatu za mchezo huo huku timu ya FGA ikiuhitaji zaidi mchezo huo jambo lililoifanya iongeze mashambulizi zaidi huku ikijilinda na hatimaye kuibuka kinara wa mchezo huo.
Magoli ya FGA yamefungwa na mchezaji Andrew Chamungu Jezi namba 7 aliyefunga magoli 2 katika dakika ya 31 na 55 na Saidiki Ramadhan aliyefunga goli 1 dakika ya 75 kwa mkwaju wa penati huku goli pekee la kufutia machozi la Mbeya City likifungwa na Arish Kombo katika dakika ya 83 ya mchezo huo.
Timu zote zimefanikiwa kubaki katika ligi hiyo kwa msimu ujao, na zote zikiahidi kufanya vizuri zaidi msimu ujao.