Katibu tawala Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Mariam Msengi akizungumza kwenye hafla fupi ya ufunguzi wa majengo mapya ya shule ya awali ya Kimataifa ya Isamilo
Muonekano wa Shule ya awali ya Kimataifa ya Isamilo inayotumia mtaala wa Cambridge iliyoko Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Isamilo iliyoko Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza wakitoa burudani kwenye hafla ya ufunguzi wa majengo mapya ya shule ya awali ya Kimataifa ya Isamilo iliyoko Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza
…………………………….
Jamii imeombwa kuacha tabia za ukatili kwa watoto ikiwemo kuwaozesha ndoa za utotoni ambazo zinawakatili kupata elimu ambayo ni msaada katika maisha yao.
Ombi hilo lumetolewa leo Alhamisi Aprili 25, 2024 na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Zephania Ntuza kwenye hafla ya ufunguzi wa majengo mapya ya shule ya awali ya Kimataifa Isamilo iliyoko Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza.
Amesema ndoa za utotoni zinawaathiri watoto kisaikolojia pamoja na kuwakatili kihisia kwani umri wao haujafikia hatua hiyo.
“Wazazi na walezi wote pelekeni watoto shule ili waweze kupata haki yao ya elimu mnapowaozesha katika umri mdogo mnawakosea,Kanisa la Anglikana linaungana na Serikali yetu kupinga ukatili kwa watoto,ndoa za utotoni na ukeketaji kwa watoto wa kike”, amesema Askofu Ntuza
Kwaupande wake Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Shule ya Kimataifa Isamilo Mchungaji Jacob Mutashi, amesema wazazi wanapaswa kuwekeza kwenye elimu kwakuwapeleka watoto wao shule kwani kwakufanya hivyo ni kujiwekea akiba itakayowasaidia uzeeni.
“Wazazi wengi wamekuwa na tabia ya kuwaozesha watoto wao kwa taamaa ya kujipatia mali jambo ambalo linakuja kuwatesa wanapozeeka kutokana na kukosa msaada”, amesema Mchungaji Mutashi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kojas Builders iliyotekeleza ujenzi wa shule hiyo Nyerere Lucas, amesema mradi huo umegharimu Milioni 800 ambapo ulihusisha majengo saba yakiwemo manne yenye Madarasa mawili,jengo la utawala,maktaba na jengo la watumishi
Awali akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda Katibu tawala Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mariam Msengi, amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki ya watoto kusoma ikiwa ni pamoja na kujenga shule mpya za msingi na sekondari,elimu bila malipo pamoja na kuboresha miundombinu.