RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Mhe.Yahya Bin Ahmad Ukeysh alipofika Ikulu Jijini Zanzibar na ujumbe wake kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo. 27-4-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Mhe. Yahya Bin Ahmad Ukeysh, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 27-4-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Mhe. Yahya Bin Ahmad Okeish, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 27-4-2024.(Picha na Ikulu)
…………………….
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali
Mwinyi ameihakikishia Serikali ya Saudi Arabia ushirikiano mzuri uliopo na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa kwenye miradi mbalimbali ya
Maendeleo.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na Balozi wa
Saudi Arabia nchini Tanzania, Mhe. Yahya Ahmad Okeish na ujumbe wake kwa
lengo la kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya nchi mbili hizo.
Dk. Mwinyi alisema, SMZ ni mnufaika mkubwa wa mfuko wa Saudia na Quwait
kwenye miradi yake ya maeneleo kupitia ushirikiano mzuri uliopo baina ya mataifa
hayo.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameishukuru na kuipongeza Serikali ya Saudi Arabia kwa
ushirikiano wake na Tanzania hususan kuipatia Zanzibar zawadi mbalimbali
inazozituma kwa watu wa Zanzibar ikiwemo tende wakati wa Mwezi mtukufu wa
Ramadhan.
Katika salamu zake kwa Tanzania, Balozi Okeish amepongeza mafanikio makubwa
yaliyofikiwa na taifa hili kwa kutimiza miaka 60 ya Muungano wake baina ya
Tanganyika na Zanzibar sambamba na kuuombea mafanikio zaidi muungano huo.
Pia, Balozi Okeish alisifu ushirikiano wa diplomasia uliopo baina ya Saudi Arabia na
Tanzania ikiwemo Zanzibar pamoja na kusifu tamaduni za pande mbili hizo.