Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania na ule wa Afrika Mashariki ukiimbwa katika Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kushuka kwenye gari Maalum la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Sherehe hizo zimefanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Sherehe hizo zimefanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024.
……………………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameongoza watanzania katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo Aprili 26, 2024 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
Katika Sherehe hizo, Mhe. Rais Samia amekagua gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kushirikiana na vikundi vya Ulinzi na usalama na kupokea salamu za utii, kisha gwaride hilo kupita kwa heshima mbele yake kwa mwendo wa pole na mwendo wa haraka.
Sherehe za maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru zimehudhuriwa na viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Burundi, Zambia, Kenya, Somaria, Namibia, Uganda pamoja na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Katika miaka 60 ya uhuru Tanzania imefanikiwa kupiga hatua katika maendeleo na baadhi ya mafanikio hayo ni : Kuulinda uhuru na mipaka, Amani; Kuimiraisha uchumi – uchumi wa kati; Kuboresha huduma za kujamii, kuimarisha demokrasia.
Tanzania, chini ya Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (1985-1995) iliruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania na kuanza mpango wa kurekebisha uchumi kuendana na masharti ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani.
Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa (1995-2005) aliendeleza mfumo wa uchumi wa soko huria ambapo mashirika ya umma yanabinafsishwa. Tarehe 21 Desemba 2005 Jakaya Kikwete aliapishwa kuwa Rais wa nne wa taifa (2005-2015), naye aliendeleza sera za watangulizi wake akitokea chama hichohicho cha CCM.
Aliyemfuata mwaka 2015 ni rais wa tano John Pombe Magufuli (CCM)aliyerudia awamu ya Pili 2020, lakini kwa mapenzi ya Mungu naye ametangulia mbele ya haki za Bwana na ambaye Watazania wanaendelea kukumbuka yote hasa urithi mkubwa aliouwacha na sifa aliyoiachia jina la Tanzania. Na rais wa awamu ya sita ni Dkt. Samia Suluhu Hassani