Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wananchi pamoja na Viongozi mbalimbali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024.
Gwaride la Heshima la Miaka 60 ya Muungano lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Viongozi mbalimbali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024
…………………
NA NOEL RUKANUGA NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendeleza Muungano kwa kutekeleza falsafa ya maridhiano, kustamiliana, kufanya kazi kwa bidii pamoja kuleta mageuzi ya kuijenga Nchi.
Akizungumza leo Aprili 26, 2024 katika Sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, Rais Dkt. Samia amesema kuwa maridhiano yatajenga amani na utulivu wa kudumu katika nchini na kuleta maendeleo endelevu.
“Leo hii tunafahari nchi yetu imefika hadhi ya uchumi wa kati ngazi ya chini na tathimini zote zinaonesha tunaweza kufikia uchumi wa kati ngazi ya juu” amesema Rais Mhe. Dkt. Samia.
Rais Dkt. Samia amesema kuwa kupitia muungano wameweza kudumisha umoja na mshikamano wa kitaifa kwa kuimarisha udugu, kupiga hatua kubwa ya maendeleo ya kiuchumi, siasa na kijamii pamoja na kudumisha mila na desturi.
Amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani ya nchi ili kujenga uchumi wa nchi na kuleta ustawi bora kwa wananchi.
“Tuna kila sababu ya kujivunia muungano wetu, kwani nchi ya Tanzania imetokana maamuzi yetu wenyewe katika kipindi chote cha miaka 60 tukiwa na makabila zaidi ya 120 wenye imani tofauti za kidini na kuunganishwa na lugha moja ya Kiswahili ambayo imeweza kudumisha nchi kuwa na amani na utulivu” amesema Rais Dkt. Samia.
Amewakumbusha watanzania kufanya kazi kwa bidii na kutumia maarifa zaidi ili kukuza tija kwa ustawi wa Taifa, kwani kazi ni kipimo cha utu.
“Uwajibu wetu ni kufanya kazi kwa bidii ili tuwezeshe upatikanaji wa haki ya msingi za binadamu na kustawisha utu wa watanzania” amesema Rais Dkt. Samia.
Amewapongeza watanzania kwa kuadhimisha miaka 60 ya Muungano kwa kushikamana na kuimarika kwa kipindi chote, huku akiwashukuru wageni wote walioshiriki katika maadhimisho hayo.
Katika Sherehe za Miaka 60 ya Muungano Mhe. Rais Samia amekagua gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kushirikiana na vikundi vya Ulinzi na usalama na kupokea salamu za utii, kisha gwaride hilo kupita kwa heshima mbele yake kwa mwendo wa pole na mwendo wa haraka.
Sherehe za maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru zimehudhuriwa na viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Burundi, Zambia, Kenya, Somaria, Namibia, Uganda pamoja na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Katika miaka 60 ya uhuru Tanzania imefanikiwa kupiga hatua katika maendeleo na baadhi ya mafanikio hayo ni : Kuulinda uhuru na mipaka, Amani; Kuimiraisha uchumi – uchumi wa kati; Kuboresha huduma za kujamii, kuimarisha demokrasia.
Tanzania, chini ya Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (1985-1995) iliruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania na kuanza mpango wa kurekebisha uchumi kuendana na masharti ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani.
Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa (1995-2005) aliendeleza mfumo wa uchumi wa soko huria ambapo mashirika ya umma yanabinafsishwa. Tarehe 21 Desemba 2005 Jakaya Kikwete aliapishwa kuwa Rais wa nne wa taifa (2005-2015), naye aliendeleza sera za watangulizi wake akitokea chama hichohicho cha CCM.
Aliyemfuata mwaka 2015 ni rais wa tano John Pombe Magufuli (CCM)aliyerudia awamu ya Pili 2020, lakini kwa mapenzi ya Mungu naye ametangulia mbele ya haki za Bwana na ambaye Watazania wanaendelea kukumbuka yote hasa urithi mkubwa aliouwacha na sifa aliyoiachia jina la Tanzania. Na rais wa awamu ya sita ni Dkt. Samia Suluhu Hassani.
Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wakiwa kwenye kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024.