Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani, yanayofanyika kila ifikapo April 25 Duniani kote ambapo kwa Zanzibar yamefanyika Hoteli ya Golden tulip Uwanja wa ndege.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazuri (kulia) akivuta Uzi kuashiria uzinduzi wa Baraza la kumaliza Malaria Zanzibar, inayoaadhimishwa kila mwaka duniani kote, ifikapo April 25 ambapo kwa Zanzibar imeadhimishwa Hotel Golden tulip Uwanja wa ndege.
Wasanii wa Ngoma ya kibati wakitoa burudani yenye yenye mnasaba wa siku ya maleria, ambayo huadhimishwa kila mwaka Duniani ifikapo April 25 ambapo kwa Zanzibar yamefanyika katika Hoteli ya Golden tulip Uwanja wa ndege.
Mkurugenzi kinga na elimu ya afya Dkt.Salim Slim akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo yanayofanyika kila ifikapo April 25 Duniani kote ambapo kwa Zanzibar hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Golden tulip Uwanja wa ndege.
Baadhi ya wadau wa mapambano dhidi ya malaria waliposhiriki maadhimisho ya siku ya malaria Duniani ambayo hufanyika ifikapo April 25 Duniani kote ambapo kwa Zanzibar maadhimisho hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa ndege.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt.Habiba Hassan Omar akimkaribisha Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazrui kuzunguma na wadau wa mapambano dhidi ya malaria katika hafla ya maadhimisho ya siku ya malaria ambayo hufanyika April 25 Duniani kote na kwa upande wa Zanzibar imeadhimishwa katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden tulip uwanja wa ndege.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akipata maelezo kutoka kwa Mtambuzi wa mifumo Nicholaus kuhusiana na ugawaji wa vyandarua kupitia mfumo wa kidigitali (Mass ITN distribution systems),ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya malaria Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo April 25 ambapo kwa Zanzibar yaliambatana na uzinduzi wa ugawaji wa vyandarua na Baraza la kumaliza malaria Zanzibar huko Hoteli ya Golden tulip Uwanja wa ndege.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akimkabidhi vyandarua mwananchi kutoka Mbweni Suleiman Suleiman mara baada ya kuzindua zoezi la ugawaji wa vyandarua katika maadhimisho ya siku ya malaria Dunia ambayo kwa Zanzibar imefanyika Golden Tulip Uwanja wa ndege.
………..
Na Fauzia Mussa. Maelezo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka viongozi wa Mikoa yenye maambukizi ya maradhi ya Malaria kutekeleza vizuri mikakati iliowekwa ili kumaliza ugonjwa huo.
Katika hotuba iliyosomwa kwaniaba yake na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani huko Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa ndege amesema ugonjwa huo unaendelea kupungua, lakini bado kuna baadhi ya maeneo hususan katika Wilaya za Mjini, Magharibi ‘A’ na ‘B’ unaendelea kuwepo.
“Hali hii haikubaliki na ninaelekeza hatua madhubuti zichukuliwe kudhibiti tatizo hilo kwa kushirikisha sekta zote nchini na hili linawezekana linataka usimamizi nzuri wa utekelezaji wa afua za kupambana na malaria.” Aliagiza Dkt. Mwinyi.
Aidha amefahamisha kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha huduma zote muhimu za Afya katika kudhibiti malaria zinaendelea kutolewa kwa wananchi wote.
Dkt. Mwinyi amewahimiza wananchi kulala ndani ya vyandarua vilivyotiwa dawa na kufika mapema katika vituo vya Afya ili kupatiwa huduma zinazostahiki pale wanapohisi dalili za ugonjwa huo.
Ameeleza kuwa ni muhimu kuzingatia maelekezo ya Wataalamu wa Afya ili lengo la kumaliza Malaria nchini ifikapo mwaka 2029 liweze kufikiwa.
Sambamba na hayo Dkt. Mwinyi ameipongeza Wizara ya Afya kupitia Programu ya kumaliza malaria Zanzibar kwa kuweza kudhibiti mripuko wa ugonjwa huo uliosababishwa na mabadiliko ya tabianchi kati ya kipindi cha mwezi Septemba hadi Disemba 2023.
Mkurugenzi Idara ya kinga na elimu ya afya Dkt. Salim Slim ameeleza kuwa kupungua kwa Maleria kumefungua fursa ya watalii kuingia nchini kwani kila mtalii anamini Zanibar ni salama kwa afya yake.
Ameipongeza Serikali kwa kuiwezesha Wizara ya Afya kuhakikisha dawa za ugonjwa huo zinapatikana na kuweka miundombinu ya barabara inapyoruhusu maji kupita jambo linaloondosha madimbwi na maji kutuwama.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Habiba Hassan Omar amesema Wizara itaendelea kuchukua juhudi za kumaliza malaria ili kuendana na malengo ya Serikali katika kupiga vita ugonjwa huo.
Aidha amewaomba wadau wa maendeleo kuendelea kuiunga mkono Serikali kwani ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali katika kumaliza ugonjwa huo Nchini.
Meneja Program ya kumaliza malaria Zanzibar Dkt. Shija Joseph Shija amesema wamefanikiwa kuudhibiti ugonjwa huo kwa kufuata Afua mbalimbali zikiwemo kudhibiti mbu wanaoeneza malaria kwa kupiga dawa majumbani, kugawa vyandarua vilovyotiwa dawa na kuuwa viluilui wa ugonjwa huo katika madimbwi pamoja na usafi wa mazingira.
Aidha wamekuwa wakifanya ufuatiliaji wa wagonjwa wa malaria majumbani kwa lengo la kubaini maambukizi katika ngazi ya familia unaofanywa na wataalamu wa ufuatiliaji wagonjwa pamoja na kutoa elimu na uhamasishaji kwa jamiii.
Nao Wadau wa maendeleo wakiwemo wawakilishi wa ALMA, USAID, WHO wamesema kuna mambo mengi ya kujivunia kutokana na mafanikio yaliopatikana na kuahidi kuendelea kushirikiana katika mapambano dhidi ya Maleria.
Aidha wadau hao wameiomba wizara ya afya kupitia program ya kumaliza malaria kuendelea kusimamia mikakati ya kujilinda na ugonjwa huo kwani mripuko uliotokea 2023 unaonesha kuwa wakati wowote ugonjwa huo unaweza kutokezea ikiwa hakutakua na tahadhari ya kutosha.
Siku ya Maleria Duniani inaadhimishwa kila ifikapo April 25 ambapo kwa Zanzibar yameambatana na zoezi la uzinduzi wa vyandarua na Baraza la kumaliza Malaria Zanzibar na kwa upande wa kaulimbiu kwa mwaka huu ni ” NIPO TAYARI KUSHINDA MALARIA ZIRO MALARIA INAANZA NA MIMI”.