Kaimu Meneja wa Utafiti na Usahuri Elekezi na Machapisho, Chuo cha Bahari (DMI) Jonnes Lugoye akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
……………………….
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM
Katika kuadhimisha miaka 60 ya Muungano Chuo Cha Bahari (DMI) kimefanikiwa kupiga hatua katika nyanja mbalimbali ikiwemo kitaaluma pamoja na kuhakikisha Tanzania Bara na Visiwani wananufaika na uchumi wa buluu
Akizungumza leo Aprili 24, 2024 katika Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa Utafiti na Usahuri Elekezi na Machapisho, Chuo cha Bahari (DMI) Jonnes Lugoye, amesema kuwa wanaendelea kutekeleza majukumu kwa uweledi ili kuleta tija kwa Taifa.
Lugoye amesema kuwa katika miaka 60 ya muungano chuo kimeendelea kupata mafanikio kadri siku zinavyozidi kwenda ikiwemo kuzalisha idadi kubwa wataalumu.
Amesema kuwa wakati chuo kinaazishwa kulikuwa na wanafunzi 12, lakini mpaka kufika mwaka huu chuo kina jumla ya wanafunzi 5,177.
“DMI ni chuo pekee kinachozalisha wataalamu wa bahari ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika maeneo mbalimbali na kulisaidia Taifa katika kukuza uchumi“ amesema Lugoye.
Amefafanua kuwa chuo kimeendelea kutoa mafunzo kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu na kuchachua uchumi wa buluu ambao unachingia katika uchumi wa Taifa kwa asilimia 30.
DMI ni Chuo ambacho kinajukumu la kutoa ushauri elekekezi kwa serikali, makapuni, kufanya utafiti na kupata fursa zilizopo katika uchumi wa buluu.
Lusajo Martin kutoka Chuo cha Bahari DMI akizungumza katika maonyesho hayo.
Daniel Rukomu mhadhiri wa Chuo cha Bahari DMI akifafanua jambo katika bandari la chuo hicho viwanja vya Mnazi Mmoja.