Na Issa Mwadangala
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Magoma amewataka wazazi kuhakikisha wanakuwa karibu na watoto wao, kujenga tabia ya kuzungumza nao ili kujua uwezo wao wa kujitambua na kuwajengea uwezo wa kufahamu athari ya ukatili wa kijinsia ili waweze kuchukua tahadhari.
Aidha, Mkaguzi Magoma alisema “Wazazi mna jukumu kubwa la kuhakikisha watoto hawafanyiwi ukatili wa kijinsia kwa kuwa na utaratibu wa kuwakagua watoto sehemu za siri ili kujua kama wapo salama pia wazazi msiwe chanzo cha watoto wa kike kushindwa kuendelea na masomo kwa kuwaozesha wakiwa na umri mdogo”
Naye, Afisa Mtendaji wa Kata hiyo ndugu Ally Nduka alitoa pongezi kwa jitihada zinazofanywa na Jeshi la Polisi katika kuzuia na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto unaofanywa katika jamii.
Pia alisema utaratibu huu wa kutoa elimu ya madhara ya ukatili utasaidia kupunguza ama kumaliza janga la ukatili dhidi ya watoto katika Kata hiyo.