Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kalaghe Kilonzo ameipongeza Kampuni ya Vodacom na Kampuni ya Lamata village kwa kuendelea kuinua tasnia ya filamu nchini.
Hayo ameyasema Aprili 24,2024 jijini kwenye ukumbi wa wa Cinemax Mlimani City Dar es salaam wakati akizindua tamthilia ya EZRA na ‘Application ‘ya Vtv lengo likiwa kusapoti kazi ya sanaa.
Amesema sanaa imeendelea kukuwa hivyo ametoa rai kwa waandaji wa filamu kuhakikisha wanatumia teknolojia katika kazi zao.
“Niliwaambia wasanii hatuna miaka miwili mbele kazi ya sanaa itakuwa imebadilika hivyo wanapaswa kujiandaa kutumia mifumo hii ya digiti”Amesema.
Ameongeza “Wapo ambao walielewa kwa haraka na wengine wanaelewa taratibu huko nyuma tulikua na usambazi wakati wa DVD lakini sasa teknolojia inabadilika”,Amesema.
Amesema kilichofanywa na kampuni ya Vodacom ni kazi iliyofanywa na wasambazaji wa DVD zamani hivyo amewapongeza kufanya hivyo hasa kwa kuangalia ‘Local Content’.
“Mlichokifanya Vodacom mmekuja kufanya kazi ambayo ilikuwa inafanywa na wasambazaji na kinachofurahisha mnaangalia Local Content wadau hawa Producers wanapokuwa na uhakika anapozalisha filamu yake papo mahala ambapo anakwenda kuuza watazalisha filamu kwa wingi mno na vipaji vipo na uwezo wa kuzalisha filamu wanao”amesema.
Amesema serikali ipo tayari kuwaunga mkono pindi watakapohitaji lakini pia inawapongeza kwa hatua hiyo kubwa.
“Tamthilia zilianza tangu miaka ya nyuma kama Rebecca,Jua kali na nyingine ambazo zinaendelea ambapo jua kali inatuzo zaidi ya 30 nadani na nje ya nchi hii ni kazi kubwa ambayo mnaifanya”,Amesema.
Amesema tamthilia ya EZRA naamini itakuwa na viwango bora hivyo serikali wanaiunga mkono na ikitokea popote watahitaji uwepo wa serikali basi wapo tayari kushirikiana nao.
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Dijitali na huduma za ziada kutoka Kampuni ya Vodacom Goodluck Moshi amesema wamejipanga kila mwaka kuhakikisha wanakua na maudhui mapya ya kitanzania ili kuhakikisha wateja hawakosi cha kuangalia.
”Lengo letu ni kuunga mkono serikali katika juhudi zake za kuahikikisha wanaiinua sekta ya filamu nchini”,Amesema.