Mkurugenzi wa biashara wa Benki
ya Stanbic Frederick Max na Afisa Mkuu Mtendaji wa Ramani (Mkurugenzi
Mtendaji), Lain Usiri, wakipeana mikono Mara baada ya kusaini Makubaliano jijini Dar
es salaam.
********
BENKI ya stanbic imeingia
Makubaliano na Kampuni ya ramani kwa lengo la kuwafikia Wafanyabiashara
wanaosambaza bidhaa mbalimbali za
viwandani kwa kuwapa mikopo na mitaji ya kuendeleza biashara zao.
Akizungumza Jijini Dar es
Salaam jana wakati wa kuingia Makubaliano hayo Mkurugenzi wa biashara wa Benki
hiyo Frederick Max ameeleza kuwa Makubaliano hayo yataiwezesha Benki hiyo
kufikisha Huduma za kibenki kwa wateja wengi Zaidi.
Amebainisha kuwa Benki
imeshatoa mikopo yenye thamani ya bilioni 50 kwa Mwaka Jana ambapo kwa Mwaka
huu ikitarajia kutoa shilingi bilioni 150 kwa ajili ya wasambazaji wa bidhaa za
viwandani.
“leo tumeingia makubaliano
na ramani ili kuweza kuwafikia wasambazaji wa bidhaa mbalimbali hii
itatuwezesha sisi kufikisha huduma zetu za kibenki kwa wahitaji wengi zaidi
kwasababu ramani tayari wanawateja wao nchi nzima na sisi tunaleta ujuzi wetu
wa masuala ya kibiashara”
“Sisi kama Benki
tunajiskia fahari na faraja kuweza kuwa nao kuhakikisha wafanyabiashara wengi
sana wanafaidika na huduma za kibenki
Kiasi ambacho tumetenga sisi
kwaajili ya uwezeshaji ni tayari tumetoa mikopo yenye hamani ya Bilioni 50
kuanzia Desemba mwaka 2023 Hadi sasa na mwaka huu tunatarajia ‘kuongeza hiyo
namba maradufu” Alisema Max
Kwa upande wake Afisa Mkuu
Mtendaji wa Ramani (Mkurugenzi Mtendaji), Iain Usiri, alisema kuwa Makubaliano
hayo yataiwezesha Benki hiyo kuwafatilia wateja wao kwa ukaribu zaidi lakini
pia yamelenga kufikisha ujumuishi wa Huduma kifedha kwa watanzania.
Pia alisema kampuni hiyo
inawapa wauzaji programu ya teknolojia ya umiliki wa kifedha ili kurahisisha
shughuli zao.
“Kwa hivyo tunazindua soko
la fedha ili benki inayofanya kazi nasi kupitia teknolojia yetu iweze kupata
data ya wakati halisi na tathmini za hatari za wauzaji wa FMCG”
Akiongeza “Kabla ya
teknolojia hii, benki hazina mwonekano wa mauzo ya wauzaji wa FMCG, hii
itawezesha taasisi za kifedha kupata data ya wakati halisi na tathmini za
hatari.”
Aliongeza kuwa hatua hiyo
inakwenda kukuza biashara ya ndani nchini na ushirikishwaji wa kifedha
Mkurugenzi wa biashara wa Benki
ya Stanbic Frederick Max akisaini Makubaliano na Kampuni ya Ramani jijini Dar
es salaam April 22,2024.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Ramani
(Mkurugenzi Mtendaji), Iain Usiri, akisaini Makubaliano na Kampuni ya ramani jijini
Dar es salaam April 22,2024.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Ramani na Benki ya Stanbic katika hafla fupi ya kusaini Makubaliano hayo.
Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya makubaliano kati ya Kampuni ya ramani na banki ya Stanbic Bank yenye lengo la kuwafikia Wafanyabiashara wanaosambaza bidhaa mbalimbali za viwandani kwa kuwapa mikopo na mitaji ya kuendeleza biashara zao.