Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa elimu kinga dhidi ya tatizo la dawa za kulevya katika _”Maadhimisho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahala Pa Kazi”_ yalianza rasmi katika Viwanja vya General Tyre vilivyopo Njiro jijini Arusha.
Maadhimisho hayo yameanza rasmi leo tarehe 23.04.2024 yatamalizika tarehe 30.04.2024. Mgeni rasmi wa Maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dotto Biteko. Kauli Mbinu ya Mwaka huu ni: _”Athari ya Mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika Usalama na Afya Kazini”_
Aidha, kuna uhusiano mkubwa kati ya tatizo la dawa za kulevya na usalama na afya mahala pa kazi. Matumizi ya dawa za kulevya yanaathiri mtu akili na mwili, hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kuathiri usalama na afya ya mtumishi mahala pa kazi.