ZAIDI ya mabinti 15,521 wanatarajiwa kupata chanjo ya dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi kwa mabinti wa miaka 9-14 katika wilaya ya Nachingwea
Akizungumza wakati uzinduzi wa kampeni Chanjo dhidi saratani ya mlango wa kizazi,mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa mabinti wa wilaya hiyo watapata chanjo wote kwa asilimia 100 ili kuokoa uhai wa mabinti hao
Moyo alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dr Samia suluhu Hassan inatoa chanjo bure kwa mabinti wote bure kwa kulinda afya za mabinti wote wa kitanzania.
Moyo alisema kuwa chanjo zinazotolewa ni chanjo salama haina madhara yoyote kwa mabinti na serikali imekuwa inatoa chanjo salama hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea kumuunga mkono Rais Dr Samia suluhu Hassan katika kuiweka jamii salama
Kwa upande wake Mratibu wa huduma za Chanjo Wilaya ya Nachingwea Rehema Kuchukua alisema kuwa binti asipopata chanjo anakuwa hatari kwa maisha yake
Kuchukua alisema kuwa kampeni ya chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi kwa mabinti itaendelea kutolewa katika hospitali 3, Vituo vya afya 5 na zahanati 44.
Alimalizia kwa kuwaomba wananchi kuwapeleka mabinti zao kupata chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi ili kuokoa maisha yao.