Katibu Mkuu UVCCM ambae pia ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) Jokate Urban Mwegelo akiweka shada la maua katika Kaburi la Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar marehemu sheikh Abeid Amani Karume huko Kisiwanduwi alipofanya ziara ya kwanza mara baada ya kuteuliwa kushika nyadhifa hiyo hivi karibuni.
Naibu katibu Mkuu wa umoja wa vijana (UVCCM) Zanzibar Abdi Mahmoud Abdi akiweka shada la maua katika kaburi la Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar marehemu sheikh Abeid Amani Karume huko Kisiwanduwi alipofanya ziara ya kwanza mara baada ya kuteuliwa kushika nyadhifa hiyo hivi karibuni.
Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa vijana (UVCCM) Zanzibar Abdi Mahmoud Abdi, Katibu Mkuu UVCCM Jocate Urban Mwegelo na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wakiomba dua katika kaburi la Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar marehemu sheikh Abeid Amani Karume huko Kisiwandui Mjini Unguja.
Vijana wa hamasa wakiwa katika mapokezi ya viongozi UVCCM Taifa huko Ghymkhana Wilaya ya Mjini.
Katibu Mkuu UVCCM Jokate Urban Mwegelo (NEC) akizungumza na Vijana wa chama cha Mapinduzi wakati wa ziara ya kwanza tangu kuteuliwa kushika nyadhifa hiyo hivi karibuni huko Ghymkhana Wilaya ya Mjini.
Naibu katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Abdi Mahmoud Abdi akizungumza na Vijana wa Chama cha Mapinduzi alipofanya ziara ya kwanza tangu kuteuliwa hivi karibuni huko Ghymkhana Mjini Zanzibar.
Baadhi ya wasanii kutoka Zanzibar na Tanzania bara wakishiriki katika mapokezi ya Viongozi wa UUVCCM Taifa huko viwanja vya Ghymkhana Wilaya ya Mjini.
……………………..
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Jokate Urban Mwegelo amewataka viongozi kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuweza kuwaunganisha pamoja Vijana na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Akizungumza mara baada ya ziara ya kwanza kisiwani Unguja kufuatia kuteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni huko katika viwanja vya Ghymkhana amesema umoja na mshikamano ni nyenzo muhimu ya kuendeleza chama na Jumuiya zake.
Katibu Jokate ambae pia ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (MNEC) amesema jukumu kubwa la vijana hao ni kuelezea mazuri yanyofanywa na viongozi wao ambao wanafanya kazi nzuri na kuvuka malengo ya ilani ya uchaguzi 2020-2025 jambo ambalo linazidisha imani kwa Wananchi na kupelekea kukipa ushindi chama hicho ifikapo mwaka 2025.
Aidha amewapongeza Vijana wa Zanzibar kwa mapokezi mazuri yanayothibitisha kuwa Uvccm ni nguzo ya Chama cha Mapinduzi sambamba na kuwataka kuitumia ofisi ya vijana kwa kujadili masula yanayowahusu na sio kupeleka fitna na uchochezi.
Akizungumzia kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar amesema Muungano huo umeweza kuleta maendeleo, umoja na mshikamano na kuahidi kudumisha, kulinda na kuenzi kwa maslahi ya vijana na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Naibu Katibu mkuu (UVCCM) Zanzibar Abdi Mahmoud Abdi ameahidi kushirikiana na viongozi mbalimbali katika ngazi ya matawi, wadi, jimbo na wilaya ili kuhakikisha vijana wote wanapata fursa mbalimbali zilizopo, pamoja na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yanayotolewa na viongozi wakuu wa kitaifa wa chama na Serikali.
Aidha amewakumbusha Vijana waliokabidhiwa nafasi mbalimbali za uongozi kuwashika mkono vijana wenzao ili kuleta maendeleo na kuwajenga kimaadili na kuweza kuwa viongozi bora wa hapo baadae.
Nao baadhi ya Vijana walioshiriki katika mapokezi hayo wamesema Vijana wanamchango mkubwa katika CCM hivyo wamewaomba viongozi hao kuwatumia na kuwapa fursa muhimu vijana hao ili kuweza kukiendeleza chama hicho na kuendelea kushika Dola.
Viongozi wa UVCCM wamefanya ziara ya kutembelea eneo la Forodhani na kukutana na Vijana wa Makachu, kudhuru kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu sheikhe Abeid Amani Karume lililopo Kisiwandui, kufanya matembezi kutoka Kisiwandui hadi Ghymkhana ambapo pia Viongozi hao walifanya mazungumzo na Vijana wa UVCCM Zanzibar.