Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila akikata utepe wakati akizindua Kampuni ya kuuza Magari ya Inchcape Automotive Tanzania katika hafla fupi ya uzinduzi huo uliofanyika Aprili 18, 2024 katika Ofisi za kampuni hiyo zilizopo barabara ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila akizungumza jambo katika hafla fupi ya uzinduzi Kampuni ya kuuza Magari ya Inchcape Automotive Tanzania iliyofanyika Aprili 18, 2024 katika Ofisi za kampuni hiyo zilizopo barabara ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya magari yanayotumia Teknolojia ya kisasa kutoka china ambayo yanauzwa na Kampuni ya Inchcape Automotive Tanzania.
………….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila amezindua Kampuni ya kuuza Magari ya Inchcape Automotive Tanzania kutoka nchini China, huku akiwahakikishia nchi ya Tanzania ni rafiki kwa kufanya biashara kutokana ina sera inayowasaidia wawekezaji kuendelea kufanya uwekezaji wenye kuleta tija.
Akizungumza jijini Dar es Salaama katika hafla ya uziduzi Kampuni ya Kuuza Magari iliyofanyika Aprili 18, 2024 katika Ofisi za kampuni hiyo zilizopo barabra ya Mwalimu Nyerere, RC Chalamila, amesema kuwa Serikali ipo tayari muda wowote kutoa ushirikano kwa wawekezaji.
RC Chalamila amesisitiza umuhimu wa wawekezaji nchini katika kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia kodi, kwani uwekezaji wenye tija lazima uendane na ulipaji wa kodi hivyo anatarajia kuwa mabalozi wazuri.
“Miradi yote ambayo Rais Dkt. Samia Suruhu Hassani anaifanya inatokana na ulipaji wa kodi, naomba msiwe wakwepa kodi na hilo mnalielewa vizuri wakiwemo mabalozi wetu Madam Ritha pamoja na Haji Manara“ amesema RC Chalamila.
Meneja wa Mauzo kikanda Kampuni ya Inchcape Automotive Tanzania, amesema kuwa kuingia kwa magari hayo nchini ni matokeo ya uhusiano endelevu wa kiuchumi kati ya nchi ya Tanzania na China katika kukuza la kimataifa.
Amesema kuwa magari wanayouza yanatumia teknolojia ya kisasa kutoka china yenye gharama nafuu ambayo hayatumii mafuta mengi.
“Lengo ni kuwapatia watanzania teknolojia mpya magari ambayo inatumia sasa“ amesema.
Katika hatua nyengin Kampuni ya Inchcape Automotive Tanzania imewatangaza Madam Rita Paulsen pamoja Haji Manara kwa mabalozi wa kutangaza magari hayo yenye chapa ya Changan Auto.