Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo la Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 60 ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Iliofanyika Mazizini Mjini Unguja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma akitoa salamu za Wizara katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo la Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 60 ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Iliofanyika Mazizini Mjini Unguja.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akitoa hatuba katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo la Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 60 ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Iliofanyika Mazizini Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi akitoa hotuba katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo la Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 60 ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Iliofanyika Mazizini Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo la Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 60 ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Iliofanyika Mazizini Mjini Unguja. (PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR)
……….
Na Sheha Sheha. Maelezo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali zote mbili zimechukuwa juhudi kubwa katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kupitia nyanja zote ikiwemo za Kiuchumi na Kijamii.
Akizungumza katika Sherehe ya uwekaji wa jiwe la Msingi, jengo la Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Magarib huko Mazizini Wilaya ya Magharibi ‘‘B’’ amesema kwa kipindi cha miaka 60 ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania, Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji imepiga hatua katika kuimarisha miundombinu ya Utoaji wa huduma kwa kujenga Ofisi za Kisasa.
Amesema ni wajibu Wananchi na Viongozi kuulinda, kuumarisha, kuuendeleza na kuudumisha Muungano huo ili kutimiza azma ya Waasisi wake na kuleta mafanikio zaidi kwa kizazi cha sasa na baadae.
Aidha amesema Serikali inaendelea kuimarisha Miundo mbinu mbalimbali ya Barabara, Maji Safi na Salama, Skuli za kisasa na Hospitali za kibingwa ili kuweka mazingira bora ya utoaji huduma sambamba na kuboresha Teknolojia ya Mifumo ya Utoaji Huduma kwa njia ya Kielektroniki.
Kwa uapande wake Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi, Hamad Yussuf Masauni amesema wanajivunia mafanikio ya Idara ya uhamiaji kwa kuimarika usalama ambalo ndio lengo la Waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Nae Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud amesema jengo hilo ni muhimu kwani litaondosha usumbufu wa ufinyu wa eneo katika Afisi hiyo.
Mapema akitoa taarifa ya Ujenzi huo, Kamishina Generali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala amesema ujenzi huo wa Gorofa 5 unatarajiwa kukamilika mwezi wa Agast mwaka huu ambapo jumla ya sh. bilioni 9.9 zinatarajiwa kutumika hadi kukamilika kwake.