Mzee Baraka Meneja Mauzo Drafco Group Ltd wa pili kutoka kulia akikabidhi taulo za kike kwa Dkt. Robert Magoma Kaimu Mganga Mkuu hospitali ya rufaa ya Amana Ilala jijini Dar es Salaam ambapo amepokea taulo (Baby Cheeky, Cuidado na Pinotex) kutoka kampuni ya Drafco Group Limited, Pia kampeni ya kuelimisha wanawake na watoto namna ya matumizi ya Taulo za watoto, akina mama na wagonjwa wenye mahitaji maalum ilifanyika kwa siku tano na kufungwa Aprili 19 , 2024 kulia ni Dkt. Idda Luhanga Mkurugenzi wa Premature Babies Organization.
Picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya taulo (Baby Cheeky, Cuidado na Pinotex) kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa, wazazi pamoja na watoto.
Dr. Robert Magoma Mganga Mkuu Amana akitoa shukurani zake baada ya kupokea msaada huo.
Dr. Idda Luhanga mkurugenzi wa Premature Babies Ogarnization akizungumza katika makabidhiano hayo
Mzee Baraka Meneja Mauzo Drafco Group akizungumza katika hafla hiyo ya kufunga mafunzo hayo na makabidhiano ya taulo za kike kwa akina mama na watoto kwenye hospitali ya Rufaa ya Amana Ilala jijini Dar es Salaam.
KAMPUNI ya Drafco Group kwa kushirikiana na kampuni ya Premature Babies leo Aprili 19, 2024 wameadhimisha cha kilele cha programu ya siku tano ya Dipper Care ambayo ilianza rasmi Aprilin15, 2024 ambayo ilikuwa na malengo ya kuelimisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya taulo kwa watoto, Wanawake na wagonjwa wenye.Uhitaji maalumu.
Akizungumza na waandishi wa habari jiini Dar es Salaam leo Aprili, 2024, katika hafla ya kukabidhi msaada wa taulo za kike Meneja Mauzo Drafco Group, Mzee Baraka akizungumza wakati akifunga kampeni ya siku tano ya Diaper Care, kuelimisha wanawake na watoto namna ya matumizi ya taulo (Baby Cheeky, Cuidado na Pinotex) za kike na kukabidhi taulo hizo kwa ajili ya wagonjwa na wazazi kwenye hospitali ya Amana Ilala jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo wamekuwa wakishirikiana na serikali kwa uchangia maendeleo ya uchumi wa taifa kwa kutumia sekta ya afya.
“Mama, Dada zetu mna nafasi kubwa sana kusaidia jamii kuweza kutumia bidhaa hizo ambazo matumizi ya bidhaa hizo humsaidia mtumiaji kuwa huru, salama na kuwa mwenye furaha wakati wote.” Ameeleza
Amesema wametoa elimu kwa watu zaidi ya 700 wajawazito, watoa huduma wa hospitali, ndugu wa wagonjwa waliopo hospitali ikiwa ni pamoja na kuwapatia dipper watoto njiti na wagonjwa wenye uhitaji maalumu wote waliopo hospitali.
Pia amesema kuwa umefanikiwa kugawa taulo zenye thamani ya shilingi milioni tano na elfu sabini (5,070,000).
Pia kampuni hizo zitawakomboa wagonjwa wanne walioshindwa kulipa gharama za matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Amana.
Pia mewakabidhi bidhaa ya taulo katoni 25 ambazo ni sawa na 35780 zenye thamani ya milioni 2,500,000/=
Kwa Upande wa mkurugenzi wa Premature Babies Ogarnization Dkt. Idda Luhanga akingumza katika makabidhiano hayo amesema kuwa wamewafikia anawake zaidi ya 200 wanaohudhuria Kliniki katika hospitali ya Amana na kutoa elimu namna ya kukabiliana na kujiepusha na kupata mtoto kabla ya muda.
“Kwa kutoa elimu hiyo tunaweza kukabiliana na kuzaa watoto njiti na kuweza kupunguza vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano.”
Kwa Upande wa Kaimu Mganga Mkuu hospitali ya Rufaa ya Amana Dkt. Robert Magoma akitoa shukurani zake baada ya kupokea msaada huo na kuomba kwa kampuni nyingine waweze kushirikiana kutoa misaada ya kibinadamu.
“Mmefanya kazi kubwa sana na mmefanya kazi ya ubinadamu Mungu awabariki, awazidishie moyo wa kujitolea isiwe kwa hospitali yetu tuu.”