*Asema Sijaridhishwa na kasi ya Mkandarasi ujenzi wa barabara hiyo amtaka kufanya kazi usiku na mchana
*Asistiza usafi wa mazingira pamoja kupanda miti na bustani ili kupendezesha jiji.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo April 18,2024 amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa BRT awamu ya tatu kutoka katikati ya Jiji hadi Gongo la Mboto.
RC Chalamila ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo ambapo amemtaka Mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha barabara hiyo kwa mujibu wa Mkataba ” Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wananchi hususani wa maeneo haya gongo la Mboto, Mkoa na Wananchi wa maeneo mengine ndani na nje ya Tanzania” Alisema RC Chalamila.
Vilevile RC Chalamila amewataka TANROAD kuanisha mipaka ili kuweza Kupendezesha mazingira ya barabara kwa kupanda miti na bustani kwa lengo la kuifanya miundombinu ya barabara ivutie
Aidha RC Chalamila amewataka viongozi wa Kata na mitaa katika Mkoa huo kusimamia usafi katika maeneo yao kwa kuhakikisha yanakuwa safi ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko kama kipindupindu ambapo amekemea makandarasi wa taka ambao hawafanyi kazi zao kwa uaminifu.
Sambamba na hilo RC Chalamila amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa wa barabara na huduma zingine za kijamii katika Mkoa huo ambapo amesema wajibu wake ni kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na inazingatia viwango na thamani ya pesa
Ifahamike kuwa gharama ya ujenzi wa mradi huo ni Tsh 231,664,120,108.93 muda wa kumaliza ujenzi ni miezi 32 ambapo ujenzi huo ulianza Agosti mosi 2022 hadi sasa mradi uko asilimia 62%