Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan atunukiwa Udaktari wa Heshima kutoka Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki, kutambua jitihada zake za kuendeleza mageuzi ya kijamii, kisiasa na kiuchumi -4R.
Katika picha chini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo tarehe 18 Aprili, 2024.
Baadhi ya Wahadhiri na Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali, baadhi ya waandishi wa habari, wanafunzi pamoja na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi Chuoni hapo tarehe 18 Aprili, 2024.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi pamoja na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi Chuoni hapo tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nchini Uturuki wakati akijiandaa kuingia ukumbini kwa ajili ya hafla ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Ankara tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu cha Ankara tarehe 18 Aprili, 2024. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Necdet Unuvar pamoja na Waziri wa Familia na Huduma za Jamii wa Uturuki Mahinur Ozdemir Goktas kushoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wageni mbalimbali, viongozi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ankara, mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo tarehe 18 Aprili, 2024.