Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa kikao na wadau wanaozalisha bidhaa zinazofunganshwa kwenye chupa na vifungashio vya plastiki kwa ajili ya kujadili kwa pamoja mikakati ya usimamizi thabiti wa uchafuzi wa mazingira utokanao na kuzagaa kwa chupa hizo, kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 17, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa kikao na wadau wanaozalisha bidhaa zinazofunganshwa kwenye chupa na vifungashio vya plastiki kwa ajili ya kujadili kwa pamoja mikakati ya usimamizi thabiti wa uchafuzi wa mazingira utokanao na kuzagaa kwa chupa hizo, kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 17, 2024. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme na
Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina
Mndeme akizungumza wakati wa kikao na wadau wanaozalisha bidhaa
zinazofunganshwa kwenye chupa na vifungashio vya plastiki kwa ajili ya
kujadili kwa pamoja mikakati ya usimamizi thabiti wa uchafuzi wa
mazingira utokanao na kuzagaa kwa chupa hizo, kilichofanyika jijini
Dodoma leo Aprili 17, 2024.
Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah
Hassan Mitawi akizungumza wakati wa kikao na wadau wanaozalisha
bidhaa zinazofunganshwa kwenye chupa na vifungashio vya plastiki kwa
ajili ya kujadili kwa pamoja mikakati ya usimamizi thabiti wa uchafuzi wa
mazingira utokanao na kuzagaa kwa chupa hizo, kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 17, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja Wadau mbali
mbalimbali mara baada ya kikao na wadau wanaozalisha bidhaa
zinazofunganshwa kwenye chupa na vifungashio vya plastiki kwa ajili ya
kujadili kwa pamoja mikakati ya usimamizi thabiti wa uchafuzi wa
mazingira utokanao na kuzagaa kwa chupa hizo, kilichofanyika jijini
Dodoma leo Aprili 17, 2024.
………
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali ipo katika hatua za mapitio ya
Kanuni za Usimamizi wa Taka ngumu za mwaka 2009 kwa lengo la
kuhakikisha wazalishaji wa chupa za plastiki wanawajibika kuhakikisha
taka zitokanazo na chupa za plastiki hazizagai kwenye mazingira.
Amesema hayo wakati wa kikao na wadau wanaozalisha bidhaa
zinazofunganshwa kwenye chupa na vifungashio vya plastiki kwa ajili ya
kujadili kwa pamoja mikakati ya usimamizi thabiti wa uchafuzi wa
mazingira utokanao na kuzagaa kwa chupa hizo, kilichofanyika jijini
Dodoma leo Aprili 17, 2024.
Kutokana na hali hiyo Mhe. Dkt. Jafo ametoa maelekezo kwa Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais kuhakikisha wataalam kwa kushirikiana
na wadau wanakamilisha kanuni hizo kabla ya mwisho wa Juni 2024 na
kusisitiza rasimu ya kwanza iwe imekamilika ifikapo wiki ijayo.
Aidha, ametoa wito kwa wadau kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni ili
zipatikane kanuni zitakazosaidia kuondoa changamoto ya kuzagaa ovyo
kwa chupa za plastiki katika mazingira yetu.
Uamuzi huo umetokana na majadiliano ya kina kati ya Serikali,
wazalishaji wa chupa za plastiki nchini na wadau wa mazingira.
Majadiliano hayo yameongzea chachu katika mapitio ya kanuni hizo.
“Imani yangu Watanzanaia wote ujumbe huu utawafikia na haya
tuliyojadiliana hapa ni maamuzi yenye maslahi mapana kwa pande zote
yaani Serikali na wadau.
“Kutokana na michango mizuri ya wadau, niwahakikishie ndugu zangu
tunakwenda kutengeneza kanuni ambazo zinatamfanya kila mzalishaji
atambue ya kwamba ukusanyaji wa chupa za plastiki unakuwa ni wa
lazima na si hiyari tena na hapo tutakuwa tumeokoa mazingira,“
amesisitiza Dkt. Jafo.
Pindi Kanuni hizo zitakapokamilika, Waziri Jafo ametoa maelekezo kwa
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
kuzisimamia kikamilifu na kuchukua hatua kwa yeyote ambaye chupa
yake itaonekana inazagaa ovyo mitaani.
Pamoja na hayo, amesema kuwa Serikali inatambua dhamira nzuri ya
uwekezaji kutoka kwa wadau mbalimbali ambao wanakuza uchumi wa
nchi lakini uwekezaji huo uendane na utunzaji wa mazingira.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme
amesema amepongeza jitihada za Waziri Jafo za kusimamia usafi wa
mazingira.
Bi. Mndeme amesema kuwa usafi wa mazingira ni jambo ambalo huvutia
watalii ambao wanakuja ahapa nchini na hivyo kuingiza kipato cha nchi.
Nae, Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi
amesema kikao ni jitihada za kutafsiri zile R nne za Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambazo ni
upatanishi, kuvumiliana na kujenga nchi 4.
Amesema masuala yanayoamualiwan kupitia kikao hicho na wadau wa
chupa za plastiki ni ya kujuenga na kuendeleza kufanya biashara huku
mazingira yakitunzwa.
”Tutakumbuka mwezi Februari hadi Machi katika Mkutano wa UNEA 6
moja ya ajenda ilikuwa ni suala la chupa za plastiki ambapo ni miongoni
mwa mambo ya kimataiga hivyo Mheshimiwa Waziri anatekeleza,”
amesema Mitawi.