Katibu mkuu wa Chama cha mapinduzi CCM Taifa Balozi Dokta Emmanuel Nchimbi anatarajia kuwasili mkoani Njombe april 18 mwaka huu kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuzungumza na wanaccm pamoja na wananchi juu ya changamoto zinazowasibu katika maeneo yao
Mbele ya vyombo vya habari Katibu wa siasa,Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Njombe Josaya Luoga amesema akiwa Mkoani Njombe Dokta Nchimbi atapokelewa mjini Makambako ambako atafanya mkutano katika eneo la kituo cha mabasi cha zamani utakaohusisha usikilizwaji wa kero za wananchi.
Pamoja na mambo mengine Luoga amezungumzia tabia za baadhi ya wanaCCM Kuanza kujipitisha kwa wanachama na kutoa zawadi katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi mkuu hapo Mwakani kwani ni kuwasumbua waliopo Mamlakani na ni Kinyume cha Kanuni.
Wananchi mkoani Njombe akiwemo God Jocob Nungwi wamesema hawako tayari kuwachagua viongozi wanaotaka kushinda kwa rushwa kwani madhara yake ni makubwa katika kipindi cha miaka mitano.
Kwa njia ya simu nimezungumza na Cassim Ephrem Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Njombe ambaye naye anaonya tabia hiyo kwa vyama vya siasa na kwamba wanaendelea kupambana navyo pamoja na kutoa elimu ya Madhara ya Rushwa katika Chaguzi.
Kukosa maendeleo ni miongoni mwa madhara ya kuchagua viongozi kwa njia ya Rushwa jambo ambalo kila mmoja anapaswa kupinga vitendo hivyo.