Wataalamu wa Wizara ya Maji na wawakilishi wa Benki ya Dunia wakikagua mradi wa maji wa Matare wilaya ya Ikungi mkoani Singida. Mradi huo umefanikishwa kupitia programu ya malipo kwa matokeo
Mradi unathamani ya shilingi milioni 328 ,na ujenzi wake umehusisha tenki la lita za ujazo 75,000 kwenye mnara wa mita sita ,pamoja na ujenzi wa vituo vya umma vya kuchotea maji tisa ,nyumba ya mtambo wa kusukumia maji (pump house ) ,karo la kunyweshea mifugo maji na mtandao wa mabomba kwa umbali wa kilometa 1.2.
Mradi umekamilika kwa asilimia 100 na unatoa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi