Na.Sophia Kingimali.
Tafiti za kidunia zimeitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchini nne zisizo na usalama wa Vivuko Barani Afrika ambazo ziko kwenye hatari Zaidi ya kukumbana na majanga ya ajali ya vyombo vya usafiri kwa njia ya maji.
Hayo yamesemwa leo April 16,2024 na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dkt Khalid Salum Mohammed wakati akifungua mkutano wa Kimataifa wa Wadau wa Usalama wa Vivuko barani Afrika, unaofanyika jijini Dar es Salaam
Amesema lengo la mkutano huo ni kuangalia sababu zinazochangia kuwepo kwa ajali nyingi baharini na katika mazingira mengine ya usafiribwa majini,na kutatua changamoto zake.
“Mkutano huu umewaleta pamoja kwa sabaubu imeonekana eneo hili halijapewa mkazi hasa katika hizi boti zinazosafiri katika mwamba mfano kutoka zanzibar unakwenda Tanga,Mombasa hii haijapewa mkazo unaostahiki na ndio maana ajali zinakuwa nyingi katika vyombo hivi na kusababisha maafa makubwa ikiwemo vifo”,Amesema.
Amesema kuna haja ya kujenga uwezo kwa watoa huduma katika vyombo hivyo ili kuweza kujua ni njia zipi waweze kupita kwa usalama lakini pia kutumia taarifa za hali ya hewa vizuri ili kujua hali ya bahari ikoje.
Aidha Dkt Khalid amezitaja aina za changamoto za ajali ambazo zinaweza kutokea kwenye njia za usafiri hususani baharini kuwa ni pamoja na ajali za moto, ajali za kuzama kwa vyombo na ajali za kuvamiwa na maharamia na watekaji ikiwemo ugaidi.
Amesema kukutana kwa wadau hao kutaongeza mbinu za kukabiliana na majanga katika bahari,mito na maziwa katika bara la Afrika.
Katika hatua nyingine Waziri huyo amewataka Wananchi wanaofanya Shughuli zao za kiuchumi ndani ya bahari na maziwa kufuata Sheria zinaoelekeza matumizi salama ya vyombo vya usafiri majini ili kupunguza ajali na madhara yanayoweza kuhepukika, kwa maisha Yao na jamii kwa ujumla.
Aidha Dk, Khalid Amesema kutokana hali ya mazingira salama na Bora ya Pwani ya bahari ya Hindi hususani Tanzania Jambo ambapo limepelekea nchi kuwa mwenyeji wa Mkutano huo.
Katika hatua nyingine Khalid Amesema wajumbe wa Mkutano huo wameadhimzia kuchukua hatua madhubuti na za pamoja zitakazo saidia kupunguza changamoto zinazopelekea kuongezeka kwa ajali nyingi kwa vyombo vya usarishaji baharini.
Vile vile DK, Khalid Amesema serikali zote mbili zinaendelea kusisitiza Wananchi wote hususani wanaotumia vyombo vya usafiri kufuata Sheria na miongozo iliyopo na kukazia kuanzia sasa kutakuwa na umakini kwa wale wote watakao kaidi kufuata Sheria za ndani na zile za Kimataifa.
Kwa upande wake muwakilishi wa mkurugenzi wa Shirika la Bahari Duniani (IMO) Vicent Job amesema shirika hilo limedhamiria kushirikiana na serikali za nchi mbalimbali katika kuhakikisha zinawekwa sheria zitakazosaidia kuwepo kwa usalama wa vyombo hivyo vya usafiri kwa njia ya maji pamoja na kukuza uchumi wa buluu.
Mkutano huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka ndani ya Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla ukiwa na lengo kutathimini hali ya usalama wa Pwani, ambapo miongoni mwa wataaalam wa maswala vyombo vya bahari wakishirikiana na Shirika la umoja wa mataifa Uhamiaji (IMO)ambao ndio waandaaji wa mkutano huo.