Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya masikini TASAF kutoka kata ya Lubonde wilayani Ludewa mkoani Njombe wamepewa mradi wa Ng’ombe 13 wa maziwa badala fedha taslimu baada ya kuona wanufaika wengi wanatumia fedha hizo kinyume cha kusudio la serikali ikiwa ni pamoja na ulevi hatua ambayo inaongeza umasikini katika kaya na utegemezi kwa taifa
Samweli Nziku ambaye ni afisa mifugo na Erick Kapinga mtaalamu wa kilimo kata wamesema serikali imeamua kutoa mradi wa Ng’ombe wa maziwa kwa wanufaika wa TASAF kata ya Lubonde baada ya diwani kuomba kuwapa mifugo badala ya fedha wanufaika kwakuwa wengi wao siku wanayopewa fedha hizo hulala nje na wengine kushinda vilabuni kunywa pombe na kisha kurejea nyumbani hadi pale tu pesa itakapoisha
Kata ya Lubonde ina wanufaika 12 wa mfuko wa kunusuru kaya masikini hivyo serikali imetoa Majike 12 na dume moja ambalo litatumika na wote huku pia akisema majukumu mengine waliyokabidhiwa ni kutoa elimu na matibabu kwa mifugo.
Kwa upande wa wanufaika akiwemo Ester Mtewele kutoka kijiji cha Mkiu wanaishukuru serikali kuja na mradi mbadala wa kuzikwamua kaya masikini kwasababu kundi kubwa la wanufaika huwa wanatumia fedha wanazopewa kinyume dhamira ya serikali.