Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kuhamasisha
Uwekezaji katika Bustani za Kijani Nchini kwa Maendeleo Endelevu
linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gaspar mkoani Dodoma
tarehe 15 Aprili 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano
na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo wakati alipowasili katika Ukumbi wa
Mikutano wa St. Gaspar mkoani Dodoma kwaajili ya Ufunguzi wa Kongamano
la Kuhamasisha Uwekezaji katika Bustani za Kijani Nchini kwa Maendeleo
Endelevu Tarehe 15 Aprili 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akiwa na viongozi mbalimbali katika Ukumbi wa Mikutano wa St.
Gaspar mkoani Dodoma alipowasili kwaajili ya kufungua Kongamano la
Kuhamasisha Uwekezaji katika Bustani za Kijani Nchini kwa Maendeleo
Endelevu. Tarehe 15 Aprili 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akifuatilia mawasilisho mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa
Kongamano la Kuhamasisha Uwekezaji katika Bustani za Kijani Nchini kwa
Maendeleo Endelevu linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gaspar
mkoani Dodoma tarehe 15 Aprili 2024. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo na kulia ni
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Bw. Kadari Singo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wanaotunza
bustani mbalimbali za miti na maua wa Mkoa wa Dodoma mara baada ya
kufungua Kongamano la Kuhamasisha Uwekezaji katika Bustani za Kijani
Nchini kwa Maendeleo Endelevu linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
St. Gaspar mkoani Dodoma tarehe 15 Aprili 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo (kulia) na
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule (Kushoto) mara baada ya kufungua Kongamano la Kuhamasisha Uwekezaji katika Bustani za Kijani
Nchini kwa Maendeleo Endelevu linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
St. Gaspar mkoani Dodoma tarehe 15 Aprili 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akizungumza na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo, Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Dodoma Adam Kimbisa namna ya kuongeza jitihada katika upandaji miti na
utunzaji mazingira mara baada ya kufungua Kongamano la Kuhamasisha
Uwekezaji katika Bustani za Kijani Nchini kwa Maendeleo Endelevu
linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gaspar mkoani Dodoma
tarehe 15 Aprili 2024.
………………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango ameagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja
na Mamlaka za Miji, Halmashauri na Majiji kuchukua hatua za makusudi
kulinda maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya Bustani za Kijani na
kuhakikisha hayavamiwi au kubadilishwa matumizi.
Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo wakati akifungua Kongamano la
Kuhamasisha Uwekezaji katika Bustani za Kijani Nchini kwa Maendeleo
Endelevu (Green Parks) lililoandaliwa na Jukwaa la Maendeleo endelevu
linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gaspar mkoani Dodoma.
ametaka maeneo hayo kupimwa na kuwekewa alama za kudumu kuonesha
mipaka yake pamoja na kuagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kutunga sheria
ndogo (by-laws) na kusimamia utekelezaji wake ili kuhakikisha maeneo ya
Bustani za Kijani yanalindwa na kutumika kama ilivyokusudiwa.
Aidha Makamu wa Rais ametoa wito kwa sekta binafsi pamoja na mashirika
na taasisi za umma pamoja na taasisi za dini kuwekeza katika uanzishaji na
uendelezaji wa Bustani za Kijani nchini kwa maendeleo endelevu. Amesema
hilo linapaswa kwenda sambamba na kuimarisha ushirikiano kati ya sekta za
umma na binafsi katika utekelezaji wa agenda hiyo muhimu. Pia amesema
makampuni binafsi na mashirika ya umma yanapaswa kujumuisha uanzishaji,
utunzaji na uendelezaji wa Bustani za Kijani kuwa sehemu ya wajibu wao wa
kurejesha kwa jamii (CSR).
Pia ametoa wito kwa Mamlaka zote za Miji, Halmashauri za Wilaya na Majiji,
kushindanisha vijana wa kitanzania kubuni bustani bora ya kijani katika Makao
Makuu ya Wilaya, Mkoa, Mji au Jiji iweje na kuagiza Waziri wa Nchi – OR
TAMISEMI na Waziri wa Nchi – OMR kushirikiana kuanzisha mashindano na
Tuzo ya Kimkoa na Kitaifa ya bustani bora za kijani katika Miji na Majiji.
Halikadhalika Makamu wa Rais ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dodoma
kuhakikisha wanaanzisha Bustani za Kijani tatu kabla ya mwisho wa mwaka
2025 ikiwemo moja ya Bustani ya Mimea kwaajili ya Tafiti za Kisayansi na
Uhifadhi (Botanical Garden). Amelitaka Jiji la Dodoma kuchukua hatua ya
kutangaza fursa ya kuwekeza katika Bustani tangulizi (pioneer green parks).
Ametoa wito kwa sekta binafsi kujitokeza kuwekeza katika kuanzisha bustani
hizo mkoani Dodoma ili pamoja na kutunza mazingira kufanya mkoa huo
kupendeza zaidi.
Amesema uanzishwaji na uendelezaji wa Bustani za Kijani ni suala linalohitaji
ushirikishwaji wa taasisi na wadau mbalimbali wenye utaalam ili kuhakikisha
uendelevu wa bustani hizo na thamani ya fedha itakayowekezwa. Makamu
wa Rais ametaja baadhi ya mambo yanayopaswa kuangaliwa kabla ya
kuwekeza ni utambuzi na uchambuzi wa mazingira ya bustani, usanifu wa
ardhi na bustani yenyewe, aina ya miti na maua yanayofaa katika eneo hilo,
kubainisha vifaa vitakavyotumika, sehemu za huduma mbalimbali kama vile
kupumzika, michezo na mazoezi, ukusanyaji wa rasilimali pamoja na mpango
kazi wa utekelezaji.
Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Dkt. Selemani Jafo amesema Mipango ya Serikali ni kujielekeza
katika uchumi wa kijani ambao unabebwa katika nguzo kuu tatu, ukuaji wa
uchumi ustawi wa jamii na utunzaji wa mazingira. Amesema uwepo wa
Kongamano hilo unaenda sambamba na lengo namba 11 na lengo 15 la
Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ambayo ni kuweka miji na makazi
ya binadamu kuwa jumuishi , salama, imara na endelevu pamoja na kulinda
uhai katika ardhi na baionuwai.