Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ametangaza kila shule lazima walime bustani za mboga mboga kwa ajili ya kutoa elimu ya lishe bora kwa faida ya taifa
Moyo aliwaambia walimu wa kata ya naipanga kutoa elimu ya lishe ili kuwa na kizazi bora chenye uwezo wa kufikiri kwa kina na kuleta maendeleo kwa taifa kwa ajili ya vizazi vya sasa na baadaye.
“Mtoto asipokuwa na lishe bora basi taifa litakuja kuongozwa na viongozi wasiokuwa na uwezo na kulipeleka taifa sehemu isiyo takiwa”
Moyo aliwaomba walimu kuendelea kutoa elimu ya lishe bora kila sehemu wanapopata nafasi ya kuongea na wananchi wowote wale.
Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo aliwaagiza wakuu wa shule na walimu wakuu kupeleka taarifa za elimu za kila mwezi ili kuboresha elimu kama ilivyokuwa swali.