Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya
Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Viwanja vya
Maonesho ya Biashara Nyamanzi Wilaya ya Magharibi ‘B’ Mkoa wa Mjini
Magharibi leo Aprili 14, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali
Mwinyi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia)
akishiriki uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara
Nyamanzi Wilaya ya Magharibi ‘B’ Mkoa wa Mjini Magharibi leo Aprili 14,
2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Katikati ni
mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji
……………………..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Dkt. Selemani Jafo amesema miongoni mwa sababu za Muungano wa
Tanzania ni udugu wa damu kati ya wananchi wa Tanzania Bara na
Zanzibar.
Amesema wananchi wa pande mbili za Muungano wameunganishwa na
lugha adhimu ya Kiswahili ambayo imejenga urafiki kati yao chini ya
waasisi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na
Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.
Dkt. Jafo amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka
60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Viwanja vya
Maonesho ya Biashara Nyamanzi Wilaya ya Magharibi ‘B’ Mkoa wa Mjini
Magharibi leo Aprili 14, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali
Mwinyi.
Akizungumzia historia fupi ya Muungano, Dkt. Jafo amesema kuwa hadi
kufikia kusaini Hati ya Muungano, viongozi hao wawili waliunganishwa na
vyama vya TANU kwa upande wa Tanzania Bara na ASP kwa upande wa
Zanzibar ambavyo vilitoa mchango mkubwa katika Muungano.
Hivyo, amesema kuwa katika kilele cha miaka 60 ya Muungano, kitabu
cha Historia ya Muungano kitazinduliwa ili kuijengea jamii uelewa zaidi
kuhusu wapi tulipotoka na wapi tunaelekea huku tukidumisha Muungano
huu adhimu.
Ametoa pongezi kwa viongozi wakuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi
kwa kuendelea kusimamia utatuzi wa hoja za Muungano katika kipindi
kifupi cha uongozi wao.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
wakiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman
Abdulla na viongozi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.
Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano yamechagizwa na kaulimbiu,
“Tumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa Letu”, ambapo
kilele kitakuwa Aprili 26, 2024 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam
ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan.