Baada ya kukaa kikao chetu na kuona kwamba kuna matatizo makubwa ambayo sasa ni kama Tabia mpya imezuka kwenye jamii, badala ya kujadili hoja, sasa kwenye mitandao yanajadiliwa matusi, lakini Kitu ambacho Si Cha kiungwana, matusi yanayojadiliwa mengi ambayo sasahivi yameshika hatamu ni kwamba mwanamke amekuwa mtu wa kutwezwa utu wake
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa JUMIKITA Bw. Shaban Omary Matwebe wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam kufuatia kashfa na matusi wanayotupiwa wanawake na viongozi wetu katika mitandao ya kijamii na baadhi ya Watanzania wenzetu ambao wamekosa heshima na uungwana lakini pia kama kwamba hawakubaliani na wazazi.
Matwebe amesema kwenye mitandao panapotokea matusi ya kuondoa utu wa mtu kwa namna ambavyo heshima na utu wake unatwezwa kutokana na kafsha au kebehi au dhalilishaji maana yake sisi kama taaisisi tuna wajibu wa kutoa mawazo yetu
Sisi kama Taasisi tumeona tuna mambo makuu mawili, ikiwemo kukemea, kuendelea kunyamaza kimya ni kwamba tunaendelea kufanya jambo liendelea pasipo na msingi maalumu
Leo Dunia nzima inapambana namna ya kumlinda mwanamke, na hakuna namna ya kulifanikisha jambo hili kama kwa kauli Moja tukikubaliana kwamba tujadili hoja, tuikosoe serikali, tuseme mahitaji ya wananchi, tuseme changamoto za wananchi ili serikali ichukue hatua na kusuluhisha na si kutumia mitandao kutukana viongozi wetu.
Serikali mwaka huu inaingia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na mwakani uchaguzi mkuu, wapo watu mbalimbali watagombea wenye jinsia ya kike, kama leo hii watatwezwa na kudhalilishwa, nani mtoto wa kike atapata ujasiri wa kwenda kuchukua fomu,? anasimamaje jukwaani kusema chochote!”