Mkurugenzi wa huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais – TAMISEMI Dkt.Rashid Mfaume amebaini ukiukwaji wa mununuzi ya vifaa ikiwemo jokofu za kuhifadia damu katika kituo cha afya Mwalugulu katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoa Shinyanga.
Dkt. Mfaume amebaini hayo hayo wakati wa kukagua shughuli za uendeshaji na usimamizi wa shughuli za Afya katika kituo cha Afya Mwalugulu Halmashauri ya Msalala mkoa wa Shinyanga akiwa ameambatana na timu ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
Dkt. Mfaume amebaini majokofu mawili yaliyonunuliwa katika kituo hicho kwaajili ya kuhifadhi damu kuwa ni majokofu kwaajili ya matumizi ya nyumbani.
“Hivi ni vifaa vimepoke;ewa bila kukaguliwa na haya wamepokea ni majokofu kwaajili ya kutunzia damu lakini kumbe ni majokofu kwaajili ya kufungia nyanya,karoti na parachichi ni matunda na wataalamu wametuthibitishia kuwa haya sio majokofu yad amu na wamepokeana huyu mzabuni tumemlipa bila kukagua tumeagiza majokofu ya kutunzia damu tumeletewa majokofu ya matunda” amesema Dkt. Rashid Mfaume
Kufuatia hatua hiyo Dkt. Mfaume ameelekeza mfamasia wa Halmashauri kuondolewa kwenye nafasi yake kwa kutoa taarifa ya uongo wakati wa ukaguzi wa vifaa huku akielekeza kuonywa kwa maandishi kwa wajumbe wa timu ya usimamizi wa shughuli za Afya ya Halmashauri (CHMT) ya Msalala.