Waziri wa habari Vijana utamadini na michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita akizungumza katika hafla ya kukabidhi majiko ya gesi kwa wajaasiriamali wa Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni mpango maalum wa Serikali kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wote na kutunza mazingira, hafla iliyofanyika Rahaleo Zanzibar.
Kamishna wa Mamlaka ya mapato ZRA Yusuph Juma Mwenda akihamasisha kudai risiti na ulipaji kodi kwa hiari wakati wa hafla ya kukabidhi majiko ya gesi kwa wajaasiriamali wa Mkoa wa Mjini magharibi, ikiwa ni mpango maalum wa Serikali kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wote na kutunza mazingira, hafla iliyofanyika Rahaleo Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, kazi, Uchumi na uwekezaji Mhe.Shariff Ali Shariff akizungumza katika Hafla ya kukabidhi majiko ya gesi Kwa wajaasiriamali wa Mkoa wa Mjini magharibi ikiwa ni Mpango WA Serikali kuhamasisha matumizi ya nishati Safi ya kupikia kwa wote na kutunza mazingira, hafla iliyofanyika Rahaleo Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, kazi, Uchumi na uwekezaji Mhe.Shariff Ali Shariff akimkabidhi jiko la gesi Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mjini Magharibi Ghanima Sheha Mbwara , ikiwa ni Mpango maalumwa Serikali kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wote na kutunza mazingira, hafla iliyofanyika Rahaleo Zanzibar.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dkt.Saada Mkuya akibadilishana mawazo na Meneja mkuu oryx Zanzibar Shuweikha Omar Khamis katika hafla ya kukabidhi majiko ya gesi kwa wajaasiriamali wa Mkoa wa Mjini magharibiikiwa ni mpango maalum wa Serikali kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wote na kutunza mazingira, hafla iliyofanyika Rahaleo Zanzibar. (PICHA NA FAUZIA MUSSA MAELEZO )
……..
Na Sheha She. Maelezo.
Zaidi ya Wanawake Wajasiriamali 100 wa Mkoa wa Mjini magharibi wamekabidhiwa Majiko ya Gesi ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa wote.
Akizungumza katika Shughuli ya kukabidhi majiko kwa Wajasiriamali hao huko Rahaleo, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Sharif Ali Sharif amesema majiko hayo yatawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Waziri Sharif amesema Nishati ya gesi ni muhimu kwa ajili ya kulinda afya za watumiaji pamoja na utunzaji wa Mazingira kutokana na kupunguza matumizi ya rasilimali ya Misitu.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum amewataka Wajasiriamali kulipa kodi kihalali ili kuwewezesha Serikali kupata mapato na kutoa huduma bora kwa Wananchi.
Naye Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita ameishukuru Kampuni ya ORYX ENERGIES kwa mchango wao wa Majiko hayo ambayo yatawarahisishia Wajasiriamali hao katika Shughuli zao na kuwakinga na madhara yatokanayo na matumizi ya kuni ikiwemo moshi.
Naye Meneja Mkuu wa ORYX ENERGIES Kanda ya Zanzibar, Ndg. Shuweikha Khamis Juma amesema Kampuni hiyo imetoa msada huo ili kuwasaidia wanawake hao kuondokana na athari zianazoweza kutokana na matumizi ya nishati ya kuni ikiwemo magonjwa mbalimbali.
Nao Wanawake Wajasiriamali walionufaika na Majiko hayo Wameushukuru Uongozi wa ORYX ENERGIES kwa kuwapatia majiko hayo na kuahidi kuyatumia Vyema ili lengo lililokusudiwa liweze kutimia.