Katibu wa Taasisi ya Majilis Almaarif Islamiyya Jamila Omar Khamis akimkaribisha Mwakilishi wa viti maalum kupitia Vijana Hudhayma Mbarak Tahir kuzungumza na watoto yatima katika hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na taasisi hiyo huko Zanzibar Park Makufuli Zanzibar.
Mwakilishi wa viti maalum kupitia Vijana Hudhayma Mbarak Tahir akila chakula cha mchana pamoja na watoto yatima kwa lengo la kuwafariji katika skukuu ya Idd el fitr huko Zanzibar Park Makufuli Zanzibar.
Mwakilishi wa viti maalum kupitia Vijana Hudhayma MbarakTahir akitoa nasaha kwa watoto yatima alipoungana nao katika Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Taasisi ya Majilis Almaarif Islamiyya huko Zanzibar Park Makufuli Zanzibar.
Kiongozi wa watoto Yatima kutoka Mtopepo Rizki daudi Haji akitoa shukrani kwa niaba ya watoto hao mara baada ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Taasisi ya Majilis Almaarif Islamiyya huko Zanzibar Park Makufuli Zanzibar. (PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR)
………
Na Takdir Ali. Maelezo. 10.04.2024.
Mwakilishi wa Viti maalum kupitia vijana Mhe. Hudhaima Mbarak Tahir amesema Serikali inajali na kuthamini machango unaotolewa na taasisi binafsi katika kusaidia watu walio katika mahitaji maalum ikiwemo mayatima na Watu wenye ulemavu.
Ameyasema hayo huko katika viwanja vya Zanzibar Part Masingini wakati wa chakula cha mchana, kilichoandaliwa na jumuiya ya Majlis Almaarif Islamia kwa ajili ya Watoto mayatima wa Mtopepo na vijiji vya jirani, ikiwa ni kusherehekea sikukuu ya Iddilfitri.
Amesema kitendo kinachofanywa na baadhi ya taasisi binafsi kula chakula cha pamoja wakati wa sikuu na futari wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni miongoni mwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha Watoto hao hawatengwi na jamii.
Aidha amewataka Wazazi na walezi kufuatilia nyenendo za Watoto wao ili kuwakinga na vitendo viovu ikiwemo udhalilishaji sambamba na kuwataka Watoto hao kutii wazazi wao ili waweze kukuwa katika maadili mema.
Kwa uapnde wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Sheikh Tahir Khatib Tahir amesema lengo la kuandaa chakula hicho ni kuweza kuwafurahisha Watoto hao na kujihisi hawatengwi katika jamii.
Aidha wamewataka watu wenye uwezo kujitokeza kuwasaidia ili kupata fadhila na rehema za Mwenyezi Mungu.
Nao wazazi na walezi walioshiriki katika Chakula hicho wamewaomba kusaidiwa Watoto wao kwani wanaishi katika hali ngumu na kushindwa kupata huduma muhimu ikiwemo chakula na mavazi