Mkuu wa wilaya ya Iringa Komredi Kheri James mapema leo amepongeza utendaji wa jeshi la Polisi mkoani Iringa kwa kuweza kudhibiti kasi ya uhalifu na kuongeza ushirikiano na jamii.
Kheri James ameyasema hayo mapema leo katika kikao kazi cha Jeshi la polisi kilicho jumuisha Maafisa, wakaguzi na askari chini ya usimamizi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa.
Akizungumza katika kikao hicho pamoja na pongezi alizozitoa kwa Jeshi la polisi, amesisitiza umuhimu wa nidhamu, uadilifu, uwajibikaji na ushirikiano miongoni mwa askari na baina ya Askari na umma.
Aidha Kheri James ameeleza kuwa Serikali inaendelea kujipanga na kujidhatiti kulijenga na kuliwezesha jeshi la polisi ili liweze kuendelea kuwahudumia Wananchi katika mazingira bora na yenye kasi ya kisasa inayochochea ufanisi.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimetunika kutathimini, kupanga na kuweka mikakati bora zaidi ya kuimarisha Usalama wa raia na mali zao katika mkoa wa Iringa.