Wafanyakazi wote wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wameshiriki futari ya pamoja katika ofisi zake zilizopo Dar es Salam, Dodoma, Kiwira Songwe, Geita, Vituo vya Mfano vya Lwamgasa & Katente na Buhemba.
Ushiriki wa futari hiyo umefanyika tarehe 8 April 2024 kwa kuwakutanisha wafanyakazi walioko Makao Makuu ya Shirika Dodoma na kwenye ofisini zengine za Shirika zilizopo mikoani.
Wafanyakazi walioko wamempongeza sana Mkurugezi Mtendaji wa STAMICO kwa kuwafuturisha kwa pamoja. Akiongea kwa niaba ya wafanyakazi wenzake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi TAMICO Bw Mohamed Kaunya amemshukuru Mkurugezi Mtendaji wa Shirika kukubali kuwakutanisha wafanyakazi wote katika futari hasa kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhani “Tunamshukuru sana MD wetu kwa moyo wa kutujali wafanyakazi wake na kutufuturisha kwa pamoja tunaomba aendele na moyo huu wa upendo na wa kuwaleta wafanyakazi kwa pamoja” Alisema Bw Kaunya.
Matukio kufuturisha yamefanyika katika ofisi na za DsM na Dodoma naya hapa Dar es Salaam na mikoa yote ambayo Shirika linatekeleza miradi yake.