Mbunge wa jimbo la Same Magharibi, David Mathayo,amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo hususani katika sekta za elimu, maji, afya na miundombinu ya barabara ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Same.
Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Same Magharibi,wakati wa uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendelea wilayani hapo,Mathayo amesema kuwa Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia inaendelea kutekeleza mipango ya maendeleo ambapo Mwenge wa Uhuru 2024 umetembelea miradi nane ambayo mingine imeshazinduliwa na mingine kuwekewa jiwe la Msingi.
Amesema Rais amewawezesha wananchi wa Same kupata huduma stahiki zitakazosaidia kupunguza changamoto wanazokumbana nazo katika shughuli zao na kwamba wanamshukuru Kwa mapenzi yake ya dhati kwa kuwadhamini na kuwapatia huduma mbalimbali za kimaendeleo kama vile maji,afya,elimu,umeme n.k
Mathayo amesema kuwa wakati Mwenge wa Uhuru ulipozindua mradi wa maji unaohudumiwa na Ruwasa ambao umegharimu kiasi Cha fedha Sh447 milioni ambao ni miongoni mwa miradi nane iliyotembelewa na mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 kwenye wilaya hiyo.
“Ukweli mradi huu wa maji wa Kata ya Mabilioni ambao unahudumia vitongoji vinne vyenye wakazi zaidi ya 3000 unakwenda kuwa chachu ya maendeleo kwa wakazi wa hapa kutokana na jiografia ya wiilaya yetu kwamba changamoto kubwa ni maji”
“Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ameona uchungu Kwa wakazi hawa na kuleta kiasi hicho Cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji mpaka leo hii Mwenge wa Uhuru mwaka huu umekuja na kupunguza kero ya ukosefu wa maji Kwa Wananchi na mimi kama kiongozi nitaendelea kupaza Sauti yangu “
Sambamba na hayo yote pia mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 zilizindua shule ya Msingi Kisima,mradi wa kikundi Cha vijana Wajasiliamali pamoja na jengo la Mama na mtoto katika Zahanati ya Hedaru vilevile Klabu ya Kupambana na Rushwa na kuweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa barabara mpya wilayani hapo.
Mathayo amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Same,pia kutoa salama Kwa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa,Ndugu Godfrey Mnzava kumfikishia kwa Mhe Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan salamu za upendo kutoka kwa wananchi wa Wilaya hiyo.
Ikumbukwe kaulimbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024 ni “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”.