Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania,Allen Mushi (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi, mshindi wa droo ya Perfect 12, Yahya Bakari ambaye ameshinda milioni 140.5.Katika hafla ya makabidhiano hayo, M-bet pia ilizindua kampeni mpya ijulikanyo kwa jina la M-Bet Likes You ambayo itawawezesha washindi mbalimbali kushinda zawadi ya kushuhudia mchezo wa fainali wa mataifa ya Ulaya nchini Ujerumani kuanzia Juni 14 mpaka Julai 14.
Mshindi wa droo ya Perfect 12, Yahya Bakari katika pozi mara baada ya kukabidhiwa Sh milioni 140.5 baada ya kushinda droo ya Perfect 12. Katika hafla ya makabidhiano hayo, M-bet pia ilizindua kampeni mpya ijulikanyo kwa jina la M-Bet Likes You ambayo itawawezesha washindi mbalimbali kushinda zawadi ya kushuhudia mchezo wa fainali wa mataifa ya Ulaya nchini Ujerumani
Mshindi wa droo ya Perfect 12, Yahya Bakari akinyoshea kidole eneo lililoandiwa kiasi cha Sh milioni 140.5 alizoshinda kupitia droo ya Perfect 12 ya kampuni ya M-Bet. Mbali ya makabidhiano hayo, M-Bet pia ilizindua kampeni mpya ijulikanyo kwa jina la M-Bet Likes You ambayo itawawezesha washindi mbalimbali kushinda zawadi ya kushuhudia mchezo wa fainali wa mataifa ya Ulaya nchini Ujerumani.
……………………….
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam.
Mbali ya kumzawadia mshindi huyo, M-Bet pia imezindua kampeni mpya ijulikanyo kwa jina la M-Bet Likes You ambayo itawawezesha washindi mbalimbali kushinda zawadi ya kushuhudia mchezo wa fainali wa mataifa ya Ulaya nchini Ujerumani kuanzia Juni 14 mpaka Julai 14.
Maoni ya Mshindi
Bakari ambaye ni mkazi wa mkoa wa Singida alisema kuwa amefurahi kutwaa kitita kikubwa cha fedha ambapo katika maisha yake hakuwa na mategemeo ya kukipata.
Alisema kuwa yeye ni mfanyabiashara mdogo na ushindi huo utamfanya kuongeza mtaji na kuwasomesha watoto wake.
“Mimi ni mfanyabiashara au wakala wa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu. Sikuwa na mtaji mkubwa, kupitia fedha ya M-Bet, nitawezza kukuza mtaji na vile vile kusomesha watoto wangu,” alisema Bakari.
Alisema kuwa ushindi wake haukuwa rahisi kwani alipitia ugumu hasa kubashiri matokeo ya mechi kati ya Chelsea na Manchester United ambapo Chelsea iliibuka mshindi wa mabao 4-3 katika dakika za mwisho.
“Sikuweza kuangalia mechi hiyo ambapo nilimpa ushindi Chelsea kwa sababu ilikuwa inacheza nyumbani. Nilipokuwa natembea, nikaambiwa kuwa Machester United inaongoza na ni dakika za nyongeza, nikaamini kuwa nimekosa mkeka huo tena kwa mechi moja tu, niliporejea kuangalia matokeo, nikaona Chelsea wameshinda, nilifurahi sana kwani hapo nikajua kuwa sasa mimi ni miongoni mwa washindi,” alisema.
M-Bet Kutoa Zawadi Zaidi
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi alimpongeza Bakari kwa kuwa miongoni mwa mamilionea na kuwaomba Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 kujarbu bahati yao kwa kubashiri na M-Bet.
Kampeni ya M-Bet Likes You
Mushi alisema kuwa M-Bet imedhihirisha kuwa ni nyumba ya washindi na mamilionea kwani mpaka sasa Watanzania kadhaa wameshindia fedha nyingi kupitia michezo yao ya kubashiri.
Wakati huo, Kampuni hiyo imezidua kampeni mpya ijulikanayo kwa jina la M-Bet Likes You ambapo zawadi kubwa ni kushinda tiketi ya kushuhudia fainali ya michuano ya Mataifa ya Ulaya iliyopangwa kuanza Juni 14 na kumalizika Julai 14 nchini Ujerumani.
Mushi alisema kuwa washiriki wanatakiwa kubashiri na M-Bet ambapo mashabiki wa soka ambao watapata likes kuanzia 1,000 watajishindia safari ya Ujerumani ambayo itagharimiwa na kampunii yao.
Alifafanua kuwa kampeni hiyo haina idadi ya washindi kwani hata wakifika 1,000, watakwenda kushuhudia mechi ya fainali tena kwa kukaa jukwaa la karibu na uwanja.
“Unachotakiwa ni kubashiri na M-Bet katika michezo yetu mbalimbali, mbali ya kuona mechi ya fainali ya Mataifa ya Ulaya, pia unaweza kushinda Televisheni ya kisasa, Simu janja ya Mkononi, laptop na sagari ya kutembelea mbuga za wanyama kama Serengeti, nawaomba mashabiki wa soka kuchangamkia fursa hii,” alisema Mushi.