Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) jimbo la Ilala Boaz Stanton akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Ustawi wa Jamii wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Salum zawadi mbalimbali kwa ajili ya watoto waliolazwa katika Taasisi hiyo pamoja na walezi wao wanaowauguza.
Katibu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kata ya Gerezani Bahvii Sarjity akitoa zawadi kwa Jamila Kibwana kwa ajili ya mtoto wake aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati viongozi hao wa UVCCM jimbo la Ilala walipotembelea JKCI leo kwa ajili ya kutoa zawadi kwa watoto waliolazwa katika Taasisi hiyo pamoja na walezi wao wanaowauguza.
Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) jimbo la Ilala wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mara baada ya kuwakabidhi zawadi mbalimbali kwa ajili ya watoto waliolazwa katika Taasisi hiyo pamoja na walezi wao wanaowauguza.