Na Mwandiahi Wetu Jeshi la Polisi Bihalamuro Kagera.
Jeshi la Polisi Wilaya Bihalamuro Mkoani Kagera katika kuhakikisha wanaaendelea kuungana na Jamii katika Mwezi Mtukufu wa Radhamani April 07.04.2024 wameungana na Jamii wilayani humo katika Iftar Maalum iliyoandaliwa na Jeshi hilo.
Akiongea katika halfa ya iftar April 07,2024 Afisa Mnadhimu namba moja Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Yusuph Daniel amesema Jeshi hilo litaendelea kushirikiana na wananchi katika kutokomeza uhalifu katika Mkoa wa Kagera ambapo amewaomba wananchi kushirikiana na Jeshi hilo.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Bihalamuro Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP- Mohamed Abdallah Juma amebainisha kuwa umekuwa ni utaratibu wa Jeshi la Polisi Wilayani humo kuungana katika matukio mbalimbali ya Kijamii ambapo amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili Wilaya hiyo iemdelee kuwa Shwari muda wote.
SSP Mohamed Abdallah Juma aliongeza kuwa endapo wananchi wataungana kikamilifu na kuuchukia uhalifu na kushirikiana na Jeshi Polisi Wilaya humo Uhalifu utakuwa historia na kuwavutia watu wengi kufika na kuwekeza katika fursa zilizopo Wilayani humo.
Sheikh wa Wilaya Bihalamuro Hamza khatibu amewataka waumini wa dini za Kiislam na kikristo kuungana kwa pamoja katika kujenga jamii yenye hofu ya Mungu na inayochukia uhalifu.
Nao Baadhi ya Wananchi wa Wilaya hiyo waliohudhuria hafla hiyo licha ya kushukuruku Jeshi la Polisi Wilaya ya Bihalamuro wameliomba Jeshi hilo kuendelea kudhibiti uhalifu huku waliomba kuendelea kuungana na Jamii Mara Kwa Mara katika matukio ya Kijamii.