NA SOPHIA KINGIMALI
KAIMU Mkuu wa chuo cha Ufundi Stadi cha Furahika kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam, Dkt. David Msuya amesema wamejipanga kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika nyanja ya elimu kwa kutoa mafunzo kwa fani mbalimbali bure.
Pia amempongeza Rais Samia kwa jitihada kubwa ambazo amezifanya katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi kwa kusimimia vema miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu, afya, barabara kwa kupeleka fedha za kutoa ili kuleta tija stahiki kwa watanzania.
Hayo ameyasema leo Aprili 8,2024,Jijini Dar es Salaam wakatati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu miaka mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
“Tangu mwaka 2021 chini ya Serikali ya Rais Samia tumekuwa tukitoa elimu bure kutokana na ufadhiri tunaoupata kutoka katika mashiriki mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia vijana ambao wamepata alama hafifu kidato cha na nne ama walioshia darasa la saba na kushindwa kuendelea na masomo kutoka na hali ngumu za wazazi au walezi wao,” amesema..
Amesema tangu wakati huo vijana 2400 wamefanikiwa kupata elimu ya kozi mbalimbali ikiwemo hoteli, IT, Udereva, umeme, ushonaji na bandari huku wengi wao wakiwa wamepata kazi na wengine wakijiri na kuondokana kwenye dimbwi la umasikini na hali ngumu ya maisha na kujisaidia wao na familia zao.
Aidha ametoa rai kwa Serikali kuendelea kutoa elimu ya ukosefu wa kinga mwilini (UKIMWI),Unyanyasaji wa kijinsia hususan vijijini ili wananchi waweze kubaliana na changamoto hizo kikamili na si kuishia jijijni Dar es Salaam pekee.
“Wiki iliyopita nilikuwa Namtumbo, ukweli ni kwamba wengi wa wananchi hajui namna na kupambana na unyanyasaji hivyo Serikali ikiongeza nguvu vijijini ukatili utapungua kwa asilimia kubwa,” amesema.
Dkt Msuya ameongeza kuwa kutokana na wengi wa wananchi hususan wanaoishi mikoani imesababishwa watu wenye ulemavu kuchukuliwa na kupelekwa jijini Dar es Salaam na kufanywa mtaji kwa kuingizwa katika biashara ya ombamba hivyo ni vema Serikali ikatunga sheria ili kuwadhibiti watu wanaofanya vitendo hivyo ambavyo ni sehemu ya ukatili katika jamii.
Wakati huo huo ametoa pendekezo kwa Serikali kuunda mabaraza ya watoto kwenye shule na wajumbe wao wawe walimu hususan wa kike ili kutoa nafasi kwa wanafunzi wanapata changamoto ya ukatili kuweza kutoa taarifa bila woga.
Naye Mwanafuzi wa chuo hicho kwa kozi ya kompyuta, Aziza Kusanga ametoa shukrani kwa Rais Samia kwa kukiwezesha chuo cha Furahika kupata ufadhiri ambao umewasaidia vijana kujiendeleza kielimu katika programu ya elimu bure.
Pia mwanafunzi Ramadhani Said, kwa upande wake amesema Rais Samia amekuwa mtetezi kwao baada ya kufanya vibaya kidato cha nne, wamepata fursa nyngine ya kupata ujuzi bure kupitia chuo cha Furahika.