Zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni moja na milioni mia tano imetengwa kwaajili ya mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kutoka makusanyo ya mapato ya ndani ya halmashauri ya manispaa ya Ilemela jijini Mwanza
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula wakati akizungumza na kikundi cha jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi UWT tawi la Kigala, Buswelu katika ukumbi wa ofisi za CCM kata ya Kirumba ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kusikiliza kero na changamoto za makundi mbalimbali ya ndani ya Jimbo hilo ambapo amewataka kuchangamkia fursa ya uwepo wa mikopo hiyo kwaajili ya kujikwamua kiuchumi
‘.. Nawapongeza kwa kuamua kujiunga katika kikundi sasa niwaombe mkisajili kikundi chenu ili muweze kunufaika na mikopo ya halmashauri, Mpaka sasa tumeshatenga fedha nyingi za kutosha kutoka kwenye mapato yetu ya ndani kwaajili ya mikopo tangu kusitishwa kwake na Serikali ili waweke utaratibu mzuri ..’ Alisema
Aidha Dkt Mabula mbali na kupokea pongezi za Rais Dkt Samia Suluhu Hasan kwa kazi nzuri ya maendeleo anayoifanya kutoka kwa wanawake hao, Ameahidi kuwachangia kiasi cha shilingi laki Saba huku laki Tano kati ya hizo ikiwa ni kwaajili ya kutunisha mfuko wao wa kukopeshana kuwaongezea mtaji sanjari na kufuatilia kero ya uharibifu wa barabara ya kutoka Buswelu kupitia Kigala kufikia Buyombe
Kwa upande wake Katibu wa kikundi hicho ambae pia ni Katibu wa jumuiya ya UWT tawi la Kigala Bi Janeth Sostenes Bida mbali na kuwapongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hasan na Mbunge Dkt Angeline Mabula kwa kazi nzuri wanazozifanya, amefafanua kuwa wakina mama hao watahakikisha wanamuunga mkono Rais Dkt Samia katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani pamoja na kumuomba Mbunge huyo kufikisha salama zao kwake kwa kazi kubwa anazozifanya ikiwemo kutekeleza miradi inayogusa moja kwa moja wanawake kama miradi ya maji, zahanati, vituo vya afya na barabara za Lami
Jackson Satta ni mjumbe wa Kamati ya siasa ya CCM kata ya Kirumba yeye amefafanua kuwa anaridhishwa na kazi nzuri inayofanya na Mbunge huyo pamoja na kuwataka wananchi kumuunga mkono na kumuombea afya njema Ili azidi kuwatumikia huku Katibu wa ofisi ya Mbunge Jimbo la Ilemela Ndugu Charles Karoli David akiwapongeza Wanawake Kwa kupata viongozi Wanawake wanaotambua kero na changamoto za wanawake wenzao akiwemo Rais Dkt Samia Suluhu Hasan na Mbunge Dkt Angeline Mabula