Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akifanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo na Mabadiliko ya Tabianchi wa Denmark Mhe. Dan Jørgensen katika ukumbi wa NEMC jijini Dodoma leo Aprili 05, 2024. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Grace Olotu na Mkurugenzi wa Sera
na Mipango Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Igans Chuwa.
Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo na Mabadiliko ya Tabianchi wa Denmark Mhe. Dan Jørgensen akizungumza wakati wa mazungo yake naWaziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo katika ukumbi wa NEMC jijini Dodoma leo Aprili 05, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiteta jambo na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo na Mabadiliko ya Tabianchi wa Denmark Mhe. Dan Jørgensen, wataalamu mbalimbali kutoka Serikali ya Tanzania na Denmark mara baada ya kufanya mazungumzo katika ukumbi wa NEMC jijini Dodoma
leo Aprili 05, 2024. Kushoto ni Balozi wa Denmark nchini Tanzania Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mhe. Mette Nørgaard Dissing-Spandet.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo na Mabadiliko ya Tabianchi wa Denmark Mhe. Dan Jørgensen mara baada ya kufanya mazungumzo katika ukumbi wa NEMC jijini Dodoma leo Aprili 05, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo na Mabadiliko ya Tabianchi wa Denmark Mhe. Dan Jørgensen, wataalamu mbalimbali kutoka Serikali ya Tanzania na Denmark mara baada ya kufanya mazungumzo katika ukumbi wa NEMC jijini Dodoma leo Aprili 05, 2024.
………
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo na Mabadiliko ya Tabianchi wa Denmark Mhe. Dan Jørgensen.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika leo Aprili 05, 2024 jijini Dodoma, viongozi hao wamejadili ushirikiano wa nchi hizo mbili katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi na mazingira kwa ujumla.
Dkt. Jafo amemueleza Waziri Jørgensen dhamira ya Serikali ya Tanzania katika kuchagiza upatikanaji wa nishati safi ya kupikia ili kukabiliana na changamoto ya ukataji wa miti ikiwa ni katika kuhakikisha hifadhi ya mazingira inakuwa endelevu.
Amemuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Denmark huku akisema utaleta mafanikio katika utekelezaji wa miradi ya mazingira.
Amemuelezea kuhusu namna Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya
Makamu wa Rais inavyokabiliana na athari za mazingira hususan
mabadiliko ya tabianchi kupitia mikakati mbalimbali.
Aidha, Waziri Dkt. Jafo ameongeza kuwa kupitia ziara ya kiongozi huyo wadau mbalimbali wa mazingira wa Tanzania watajifunza masuala mbalimbali hususan ya Amewaomba Watanzania kutumia wigo wa fursa zinazotokea kutokana
na diplomasia ya uchumi iliyojengwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia ziara zake katika mataifa mbalimbali.
Kwa upande wake Waziri Jørgensen amesema ni wakati sasa wa
kudumisha uhusiano wa nchi hjuzo mbli ili kupambanana na mabadiliko ya tabianchi yanaikabili dunia.
Amesema kuwa mabadiliko ya tabianchi yana athari kubwa katika nchi mbalimbali duniani ikwemo Tanzania na kuathiri shughuli za kiuchumi husausan kilimo hivyo ni muhimu kuunganisha nguvu kukabiliana nayo. Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Mazingira Bi. Kemilembe Mutasa, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Ignas Chuwa, Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Dkt. Paul Deogratius Paul (kutoka Ofisi ya Makamu
wa Rais).