Mkurugenzi wa New Faraja Center Zamda Juma akikabidhiwa vyakula mbalimbali na Mhandisi Christopher Nguma Mhandisi Mkuu Mkoa wa Kinondoni Kusini ( aliyewakilisha uongozi wa TANESCO Mkoa huo katika kituo hicho kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam.
Wawakilishi wa watoto kutoka Kituo cha kulelea watoto yatima cha Faraja kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam wakipokea zawadi za vyakula mbalimbali kutoka kwa Mhandisi Christopher Nguma Mhandisi Mkuu Mkoa wa Kinondoni Kusini ( aliyewakilisha uongozi wa TANESCO.
Mkurugenzi wa New Faraja Center Zamda Juma kushoto na Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja kutoka TANESCO mkoa wa Kinondoni Kusini Samia Chande wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto mara baada ya kukabidhiana msaada huo.
……………………
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kinondoni Kusini umewapa tabasamu watoto wanaolelewa na Kituo cha New Faraja kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam kwa kuwapa vyakula ambavyo vitawasaidia kwenye kufuturu pamoja na sikukuu ya Eid.
Akizungumza mara baada ya kutoa msaada huo Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja kutoka TANESCO mkoa wa Kinondoni Kusini Samia Chande, amesema wamewafikia watoto hao kuwafariji na kuwafanya wawe na furaha muda wote.
Mkurugenzi wa New Faraja Center Zamda Juma amelishukuru shirika hilo kwa upendo wa dhati waliouonesha kwa watoto hao.
Amesema Kituo hicho kina watoto 72 na wanasoma kuanzia Chekechea, Shule ya msingi ,Sekondari na mtoto mmoja yuko Chuo huku akieleza kuwa watoto hao wanawapata kupitia ustawi wa Jamii ambapo wakiwapata wanawapeleka kwenye vituo vya kulelea watoto vilivyosajiliwa na serikali.