Maofisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali Wilayani Songwe wametakiwa kuendelea kujenga ushirikiano na wananchi na kutoa huduma bora ili kujenga imani kwa Wananchi wanaowahudumia.
Kauli hiyo ilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Agustino Senga wakati alipofanya baraza na askari wa Wilaya hiyo April 04, 2024 baada ya ukaguzi wa kazi mbalimbali za Jeshi la Polisi.
Kamanda Senga pia aliwataka askari Polisi wanapotekeleza
majukumu yao kuzingatia weledi na uadilifu ili kuleta matokeo chanya ndani ya Jeshi la Polisi.
Baraza hilo lilifanyika baada ya kufanya ukaguzi na kukagua gwaride kwa lengo la kuangalia utimamu wa askari wa Wilaya
hiyo.