RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Balozi Mdogo wa Oman Anayefanyia kazi zake Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi wakati akiwasili katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar, kuhudhuria hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Ubalozi Mdogo wa Oman Zanzibar jana 4-4-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Viongozi wa wageni waalikwa baada ya kumalizika kwa hafla ya Iftari maalum iliyoandaliwa na Ubalozi Mdogo wa Oman Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar jana 4-4-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum na Balozi Mdogo wa Oman anayefanyia kazi zake Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi, baada ya kumsalizika kwa Iftari maalum iliyoandaliwa na Ubalozi Mdogo wa Oman Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar jana 4-4-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongozana na Balozi Mdogo wa Oman anayefanyia Kazi zake Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi (kushoto kwa Rais) na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa, baada ya kumalizika kwa hafla ya Iftari maalum iliyoandaliwa na Ubalozi Mdogo wa Oman Zanzibar, katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar jana 4-4-2024.(Picha na Ikulu)
………………….
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Zanzibar na Oman.
Rais Alhaj Dk.Mwinyi amesema hayo leo katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar, Mhe.Said Salim Al Sinaw iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 04 Aprili 2024.
Kwa upande mwingine Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali ya Oman imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuisaidia Zanzibar katika miradi ya Maendeleo ikiwemo ukarabati wa majengo ya kihistoria, Afya na Elimu.