Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Ndg. Jokate Urban Mwegelo akizungumza wana-CCM wa Dar es salaam baada ya kupokelewa kwa nderemo na vifijo katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa wa Dar Es Salaam Leo April 05, 2024.
Naibu Katibu mkuu wa CCM bara John Mongera amewataka vyama vya siasa vya upinzani kutumia 4R katika kufanya shughuli zao za siasa ili kuendelea kufanya siasa za kistaarabu huku wakiwa wamejipanga kuhakikisha katika chaguzi zijazo wanashinda kuanzia ngazi ya serikali ya mtaa mpaka serikali kuu.
Hayo ameyasema leo Aprili 5,2024 jijini Dar es salaam wakati wa mapokezi ya viongozi wa chama hiko katika ngazi mbalimbali ikiwemo katibu wa itikadi uenezi na Mafunzo,katibu mkuu UVCCM na katibu mkuu wa Jumuiya ya wazazi.
Amesema uteuzi uliofanya na mwenyekiti wa chama hiko ambae pia ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan kwa viongozi hao ndani ya chama unaonyesha taswira halisi ya uongozi wake na utendaji wake.
Amesema Jumuiya zote za CCM zimeimarishwa hivyo katika uchaguzi wa serikali za mataa na serikali kuu wamejipanga vizuri huku akitoa rai kwa vijana kutokukubali kutishwa kwani chama kipo imara hivyo wakilinde na kukitetea.
“Hii safu ni ujumbe tosha kama kuna mtu alikua hamjui Rais Samia kwa safu hii lazima watamuelewa chama hakina hakina namna nyingine zaidi ya kusimamia maendeleo ya nchi na kwa kasi yake ya kutatua changamoto za wananchi basi inatosha kuonyesha utendaji wake uliotukuka”Amesema Mongera
Kwa upande katibu mkuu wa vijana Joketi Mwegelo amesema uteuzi alioupata umempa fursa ya kuweka historia ndani ya Jumuiya kwa kuwa mwanamke wa kwanza mtendaji katika Jumuiya hiyo hivyo ameahidi kuhakikisha anahakikisha vijana wanakuwa imara na kukilinda na kukitetea chama popote.
“Tutatafuta na kuzilinda kura kwa ulinzi imara na sisi kama vijana hatutakaa nyuma tutashiriki pia kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi ya serikali ya mtaa mpaka serikali kuu”,Amesema Mwegelo.
Naye,Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wazazi Alli Hapi amesema utayari wake katika kuitumikia nchi na chama hauna mashaka hivyo ameahidi kushirikiana na wengine katika kuhakikisha wanakiletea ushindi chama cha Mapinduzi CCM.
“Niwahaidi Jumuiya ya wazazi tutakwenda kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha tunaijenga upya jumuiya yetu lakini pia tupo tayari kwa mapambano niwape salam upinzani wasitegemee huruma uchanguzi ni kazi twende kwa wananchi tukatafute kura”,Amesema Hapi.
Hata Hivyo Katibu wa itikadi,uenezi na Mafunzo Amosi Makala amesema yupo tayari na amejipanga vizuri kuhakikisha anakijenga chama huku akitoa rai kwa wapinzani kufanya siasa za hoja na yupo tayari kujibu hoja na si vioja.
Nao viongozi wa umoja wa bodaboda na bajaji pamoja na viongozi wa Machinga mkoa wa Dar es salaam wamepongeza uteuzi wa wagombea hao huku wakiamani utaenda kuendeleza umoja uliokuwepo na kuwaunganisha.
Kikao cha Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi chini ya mwenyekiti wake Rais Dk Samia Suluhu Hassan kiliwateua watendaji hao ndani ya chama ili kuhakikisha wanawatumikia chama chao na kuhakikisha wanashinda kwa kishindo katika chaguzi zijazo.