Mkurugenzi udhibiti wa dawa Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) Dkt.Yonah Mwalwisi akizungumza kwenye warsha iliyowakutanisha wadau wa bidhaa za tiba Kanda ya ziwa
Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dkt.Thomas Rutachunzibwa akizungumza kwenye warsha ya siku moja iliyowakutanisha wadau wa bidhaa za tiba Kanda ya Ziwa
Katibu wa chama cha waagizaji Tanzania (TAPI) Abbas Mohammed akielezea namna wanavyoshirikiana na TMDA katika kutekeleza majukumu yao
Wadau wa bidhaa za tiba kutoka Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) kwakushirikiana na Shirika lisilolakiserikali Management Science for Health (MSH) chini ya mradi wa MTaPS wamewakutanisha wadau wa bidhaa tiba Kanda ya ziwa kwa lengo la kukumbushana sheria na taratibu za uingizaji wa dawa hususani dawa zinazotumika kwenye masuala ya afya ya uzazi mama na mtoto.
Warsha hiyo ya siku moja imefanyika leo Alhamisi Aprili 04, 2024 Katika Hoteli ya Victoria Palace Jijini Mwanza.
Mkurugenzi udhibiti wa dawa Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) Dkt. Yonah Mwalwisi, amesema dhumuni kubwa la warsha hiyo ni kuangalia dawa ambazo anazitumia mama wakati wa ujauzito na mtoto anapokuwa amezaliwa na zile anazozitumia mtoto kabla ya kufikia umri wa mtu mzima ili kuhakikisha dawa hizo zinakuwa bora na salama kwa afya ya uzazi mama na mtoto.
“Warsha hii inalenga pia kuwakumbusha wadau na wateja wetu mambo ya kuzingatia katika usajili uingizaji na usambazaji nchini bidhaa za tiba hususani za afya ya uzazi”,
Amesema kupitia warsha hiyo wadau wanaohusika na uingizaji na usambazaji wa bidhaa za tiba nchini wataongezewa uelewa kwenye dawa za binadamu,Mifugo,chanjo,dawa zenye viambata vya asili ya kulevya pamoja na vifaa tiba.
Kwaupande wake Mshauri Mkuu wa masuala ya udhibiti wa dawa,bidhaa tiba na usalama wa dawa na chanjo kutoka MSH chini ya mradi wa MTaPS Dkt.Betty Maganda amesema, mradi huo una madhumuni ya kuhakikisha ubora wa bidhaa za dawa na vifaa tiba unaongezeka hasa katika nchi za afrika.
“Matarajio makuu ni kuhakikisha kunakuwa na uboreshwaji wa upatikanaji wa dawa bora na vifaa tiba katika nchi za afrika hususani Tanzania” amesema Dkt.Maganda
Aidha, ameeleza kuwa kwenye Mamlaka za udhibiti wanawasaidia kuongeza nguvu katika kuwafikia wadau wa dawa na vifaa tiba ili waweze kuelewa utaratibu mzuri wa kuingiza dawa bora ambazo hazitaleta madhara kwa wananchi
Naye Katibu wa chama cha waagizaji Tanzania (TAPI) Abbas Mohammed ameishukuru TMDA kwanamna wanavyofanya kazi kwa ukaribu ikiwemo kutatua changamoto zao kwa wakati.
Awali akizungumza kwenye warsha hiyo Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Thomas Rutachunzibwa ametoa rai kwa wadau wa bidhaa tiba kuendelea kuwa wazalendo katika kuingiza bidhaa ambazo ni salama na zenye viwango ambavyo vimewekwa na Mamlaka ya udhibiti wa Kitaifa na Kimataifa.