MKURUGENZI Mkuu,Tume ya TEHAMA Nchini,Dkt Nkundwe Mwasaga akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi,Tume ya Tehama,Professa Leonard Mselle akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha.
…………
Na Happy Lazaro, Arusha
MKURUGENZI Mkuu,Tume ya TEHAMA Nchini,Dkt Nkundwe Mwasaga amesema Katika ulimwengu wa sasa, mageuzi ya kidijitali (digital transformation) ni nguzo kuu ya kuwezesha uchumi wa kidijitali (Digital economy) yanayokwenda sambamba kuongeza ufanisi,mapato na hata kukuza ubora wa bidhaa na huduma mbalimbali .
Mwasaga ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa siku mbili wa Jukwaa la tatu la Usalama wa Mitandao Nchini{Cybersecurity Forum} Jijini Arusha lililoshirikisha,Wawakilishi kutoka Wizara, Idara, Taasisi na Wakala mbalimbali za Serikali, Wawakilishi kutoka makampuni mbalimbali,Washirika wa Maendeleo na Mashirika yasiyo ya Kiserikali.
Amesema binadamu ambao ni watumiaji wakuu wa huduma za kidigital na walaji wa huduma ya bidhaa zitokanazo na TEHAMA wanakuwa na utayari wa kutumia TEHAMA ili kuleta mabadiliko na kuongeza ufanisi katika shughuli za kila siku.
Mkurugenzi huyo amesema kidijitali inajengwa na msingi wa dhana kuu mbili ikiwemo kutumia teknolojia za kidijitali yaani “digitization” katika shughuli zetu ili kuongeza ufanisi, mapato na hata kukuza ubora wa bidhaa na huduma na pili ni mabadiliko ya tabia za binadamu yaani“change of human behavior”. Dhana na dhana hizo mbili haziwezi kufanikiwa endapo mifumo ya kidijitali itatishia usalama wa nchi, itakuwa kikwazo kwa ukuaji Uchumi, itatishiaukuaji wa biashara za makampuni na zile shughuli za mtu mmoja mmoja.
Amesema matumizi sahihi ya mifumo ya kidijitali kunaweza kupelekea kutwezwa kwa utamaduni wa taifa na utu wetu kwa kuruhusu taarifa za siri za Serikali, Kampuni na hata zile za mtu binafsi kupatikana kwa utaratibu usio sahihi na kutumiwa na watu wasiokuwa na dhamana kwa utaratibu usio sahihi,hivyo, malengo ya mageuzi ya kidijitali hayawezi kufikiwa endapo suala la usalama wa mitandao linalowezesha matumizi salama ya huduma za kidijitali halitapewa uzito unaoendana na kasi ya maendeleo ya TEHAMA.
Mkurugenzi Mkuu ameendelea kusema Mikutano ya aina hii, hasa huu wa usalama wa mitandao ni chachu kubwa ya kuendelea kuhamasishana,kukumbushana na kubadilishana uzoefu na mawazo juu ya hatua stahiki ambazo sisi sote katika nafasi zetu mbalimbali za kitaalam na kijamii tunatakiwa kuchukua ili kuwa na dunia salama katika ulimwengu wa kidijitali.
Aidha kwa kutambua umuhimu wa kuhakikisha kuwa Tanzania iko katika nafasi salama katika ulimwengu wa kidijitali, taasisi ya Tume ya TEHAMA ambayo ina jukumu la msingi la kukuza maendeleo ya TEHAMA, imeona ni vema wadau wote mkutane kwa siku mbili hizi mfanye tathmini ya utekelezaji wa mikakati mbalimbali na kutoa ushauri pamoja na mwelekeo wa matumizi salama ya mitandao ya kompyuta na huduma za kielektroniki kwa ujumla.
Naye Mwenyekiti wa Bodi,Tume ya Tehama,Professa Leonard Mselle amesema kuwa Dunia iko katika mfumo wa kidigital hivyo ni lazima kama nchi inapaswa kubadilika na kuingia katika teknolojia kwani shughu nyingi za kijamii,biashara,kiserikali na binafsi ziko kidigital.