Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Nadir Abdullatif Alwardy akizungumza na Wananchi na Wanafamilia baada ya kumalizika kwa Dua ya kumuombea Marehemu Said Washoto Muasisi wa Mapinduzi Ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa, Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume,hafla iliofanyika Mndo Wilaya ya Magharibi A Unguja.
Muakilishi wa Familia Mfaume Said Washoto akizungumza baada ya kumalizika kwa Dua ya kumuombea Marehemu Said Washoto Muasisi wa Mapinduzi Ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa, Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume,hafla iliofanyika Mndo Wilaya ya Magharibi A Unguja.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Nadir Abdullatif Alwardy akiitikia dua pamoja na Wananchi na Wanafamilia ya kumuombea Marehemu Said Washoto Muasisi wa Mapinduzi Ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa, Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume,hafla iliofanyika Mndo Wilaya ya Magharibi A Unguja.
……….
Ibrahim Dunia. Maelezo.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui amesema Serikali inatambua michango mkubwa wa wazee walioshiriki katika kuikomboa nchi ambao wameshatangulia mbele ya haki.
Akizungumza kwa niaba yake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Nadir Abdullatif Yussuf Alwardy huko Mndo Wilaya ya Magharibi ‘‘A’’ katika muendelezo wa Dua ya kumuombea muasisi wa Mapinduzi marehemu Said Washoto Mnyuke amesema Serikali ipo bega kwa bega na Familia ya Marehemu huyo na kuahidi kuendelea kuwa pamoja katika shughuli zote za kitaifa.
‘‘Serikali kila mwaka na kila siku inawakumbuka wazee wetu wote waliopo hai na waliotangulia kwani ndio waliotukomboa na walioshiriki kwenye mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 basi wote tunawatambua na tunawaombea dua’’ Alisema Mhe. Nadir
Amesema amani yote iliyopo nchini inatokana na wazee waliojitolea kwa hali na mali kupigania nchi kwa kutafuta usawa na kudumisha amani na utulivu.
Muwakilishi wa Familia hiyo Mfaume Said Washoto ameishukuru Serikali kwa kuweka utaratibu wa kila mwaka kwa kuwaombea dua wazee wao kwani kufanya hivyo ni kuthamini juhudi na mchango wa mzee wao waliochukuwa wakati wa uhai wake.
Aidha amewashukuru wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye dua hiyo na kusema maombi ya wengi Mwenyezi Mungu anayabariki kwa haraka.
Marehemu muasisi Said Washoto amezaliwa tarehe 17.03.1933 na kufariki dunia tarehe 24/10/1986 na kuzikwa kijijini kwao Mndo tarehe 25/10/1986 Wilaya ya Magharibi ‘‘A’’.