Na Joel Maduka,Geita
Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale ,Grace Kingalame amesema nia ya Serikali ni kuendelea kushirikiana na taasisi za kidini kwa lengo la kuletea amani na utulivu kwa Taifa lakini pamoja na kuwajenga watu wake kuwa na maadili mema.
Kingalame amesema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Martine Shigela kwenye shughuli ya kuwekwa wakifu kanisa la AICT Ihega lililopo Kata ya Bukoli Wilayani geita.
Amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani nia yake ya dhati ni kuona watu wanakuwa na uhuru wa kuabudu na kumtumikia Mungu jambo ambalo litasaidia kuongeza jamii ya watu wenye maadili mema na wenye Ofu ya Mungu.
“Ni nia ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani kuendelea kushirikiana kwa dhati kabisa na taasisi za dini ikiwemo hii ya AICT na niwahakikishie kama serikali ya Mkoa wa Geita ipo tayari kushirikiana na nyinyi katika shughuli zote zinazompa Mungu utukufu”Grace Kingalame Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale.
Kingalame ameongeza kuwa Serikali inawategemea sana watumishi wa Mungu ambao wameendelea kulifanya taifa la Tanzania Kuwa salama na kwamba ni vyema kuendelea kuwafundisha watu kujua umhimu wa Mungu na kuwafundisha kweli ambayo itawaweka salama katika kumjua Mungu.